Kwa kushiriki Atabatu Abbasiyya tukufu: Ataba ya bibi Maasuma (a.s) yafanya mkutano wa tatu wa Ataba na Mazaru tukufu katika ulimwengu wa kiislamu..

Sehemu ya mkutano
Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki katika kikao cha tatu cha maandalizi kilicho fanyika katika Ataba ya Bibi Maasuma (a.s) katika mji wa Qum, kilicho hudhuriwa na wawakilishi wa Ataba na Mazaru tukufu katika ulimwengu wa kiislamu, kikao rasmi cha maandalizi ya kongamano la pili la Ataba na mazaru tukufu litakalo fanyika katika Atabatu Husseiniyya tukufu mwishoni mwa mwezi wa Rajabu sambamba na kumbukumbu ya Mab’ath (kupewa utume).

Atabatu Abbasiyya tukufu imewakilishwa na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na mkuu (mushrifu) wa kitengo cha habari na utamaduni Sayyid Adnani Mussawiy, kikao kilijikita katika kujadili kanuni za kufaya kazi kwa pamoja wawakilishi wa Ataba na Mazaru tukufu katika ulimwengu wa kiislamu, na maoni yaliyo wasilishwa yakapigiwa kura baada ya majadiliano marefu na kufikia maamuzi ya pamoja, halafu kikafanyika kikao cha jioni kwa ajuli ya kusikiliza maazimio na mapendekezo mbalimbali.

Kumbuka kua kongamano la kwanza la Ataba na Mazaru katika ulimwengu wa kiislamu lilifanyika katika mji mtukufu wa Mash-hadi na kuhudhuriwa na wawakilishi wa Ataba na Mazaru tukufu. Washiriki wa kongamano hilo walisisitiza umuhimu wa kufanyika kwa kongamano kama hilo mara nyingi zaidi, kwa ajili ya kutambuana na kubadilishana uzoefu kwa watumishi wa malalo matukufu ya Ahlulbait (a.s), kufanyika kwa vikao hivi kunaonyesha namna linavyo tiliwa umuhimu swala hili na kuhakikisha linatoa matunda mazuri ambayo yatadhihiri katika kuboresha huduma kwa watu wanaokuja kufanya ziara kwenye maenyeo haya matukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: