Kikosi cha Abbasi (a.s) kimetangaza kuukomboa mji wote wa Badushi kutoka mikononi mwa magaidi ya daesh na wamepandisha bendera za Iraq juu ya majengo ya mji huo, na kuurudisha rasmi katika himaya ya serikali kuu ya Iraq baada ya kua mikononi mwa Daesh.
Viongozi wa kikosi hicho wamesema kua: “Baada ya vita kali iliyo endeshwa na wapiganaji wa kikosi hiki wakishirikiana na kikosi cha 36 na wale wa kikosi cha tisa cha jeshi la serikali, wamefanikiwa kukomboa mji wote, na kuua makumi ya magaidi wa Daesh, sasa hivi wanajeshi wanafanya kazi ya kusafisha mji kwa kutegua mabomu ya aridhini yaliyo achwa yametegwa na magaidi hao.