Atabatu Abbasiyya tukufu yatangaza tarehe ya kuzindua mradi wa upanuzi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) upande wa upauaji wa uwanja wa haram utakua siku wa kuzaliwa kwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s)..

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetangaza kukamilika maandalizi yote ya kuzindua moja ya miradi yake mikubwa ambayo ni mradi wa upanuzi wa haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika upande wa upauaji, uzindizi huo utafanyika sambamba na kumbu kumbu ya kuzaliwa kwa mbora wa wanawake wa ulimwenguni bibi Fatuma Zaharaa (a.s) jioni ya Juma Mosi (19 Jamadil Aakhira 1438 h) sawa na (18 Machi 2017 m) baada ya swala ya Isha.

Kamati ya maandalizi ya swala hili imesema kua: “Maandalizi ya hafla ya uzinguzi yamekamilika muda si mrefu, tayali tumechakua sehemu muafaka ya kufanyia hafla hiyo, ambayo itakua ni eneo la uwanja uliopo mukabala na mlango wa Qibla katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa sababu unauwezo wa kuingiza watu wengi”.

Wakafafanua kua: “Hafla itapambwa na wazungumzaji, waimbaji wa Qaswida na mashairi pamoja na kuonyesha filamu inayo elezea hatua za ujenzi wa mradi huu, hafla itahitimishwa kwa kutolewa tangazo rasmi la kuanza historia mpya ya jengo jipya la kihistoria la Ataba ya Abulfadhil Abbasi (a.s) iliyo andikwa na watumishi wa Ataba kwa herufi za nuru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: