Maktaba na Daru Makhtutwati ya Atabatu Abbasiyya wafanya maonyesho ya utunzaji wa nakala kale kwa kushirikiana na kituo cha Dhiqaar cha masomo ya historia na uzarendo katika chuo kikuu cha Dhiqaar..

Maoni katika picha
Kituo cha ukarabati wa nakala kale na kituo cha upigaji picha wa nakala kale vilivyo chini ya ofisi ya Daru Makhtutwati katika Atabatu Abbasiyya tukufu wamefanya maonyesho ya mwaka ambayo ni ya kwanza ya utunzaji wa nakala kale na vifaa vya kiiraq kwa kushirikiana na kituo cha masomo ya historia na uzarendo cha chuo kikuu cha Dhiqaar.

Maonyesho yamefanyika katika ukumbi wa katikati ndani ya jengo la Chuo, katika maonyesho haya zimeonyeshwa nakala kale zilizo fanyiwa marekebisho na kituo cha kurekebisha nakala kale cha Ataba tukufu pamoja na majarada ya (laki) ya vioo, na baadhi ya vifaa vya kikemia vinavyo tumika katika kurekebisha nakala kale na vitabu, pia wameonyesha aina mbali mbali za wadudu na sababu zinazo pelekea kuharibuka kwa vitabu na nyaraka kwa ujumla.

Sayyid Nurudini Mussawiy mkuu wa ofisi ya Daru Makhtutwati katika Atabatu Abbasiyya tukufu aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika wazo la kufanyika kwa maonyeshi haya linaumuhimu mkubwa kwa sababu nyingi, kwanza ni kukitambulisha kizazi cha sasa hususan ndugu zetu wanafunzi umuhimu wa turathi za nakala kale na vilivyomo ndani yake ambavyo ni hazina kubwa ya elimu na tamaduni za kiiraq, hali kadhalika kutambulisha vifaa vinavyo tumika katika kurepea nakala kale na namna ya kuzitunza pamoja na kuwaonyesha ujuzi mpya unaotumika wa kuzipiga picha”.

Naye mkuu wa kituo cha masomo ya historia na uzarendo wa chuo cha Dhiqaar Dokta Shaakir Hussein Damdum alisema kua: “Kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu tumefana maonyesho haya ya mwaka ya kwanza, ambayo tunaonyesha nakala kale na namna ya kuzitunza kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo ya utunzaji wa kawaida, upigaji wa picha za kisasa na namna ya kurepea vitabu na nyaraka zingine, hakika maonyesho yametoa picha ya aina yake, yameonyesha namna ya kutunza nakala kale kwa kutumia teknolojia ya kisasa katika kuhifadhi turathi za Iraq za kihistoria ambazo zilipuuzwa na kuibwa hasa mwishoni mwa utawala uliopita (wa Sadam) kutokana na kukosekana kwa amani na usimamizi wakati huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: