Mwaka umafika tangu kuwasili kwa dirisha lililo tengenezwa na wairaq na kuwekwa juu ya kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s)..

Maoni katika picha
Mwaka umeisha tangu kufanikisha zao la ufundi wa wairaq, kuanzia kutengeneza hadi kuweka katika kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s), miezi kumi na mbili iliyojaa baraka na dua za malaika watukufu waliopo katika kaburi la kiongozi mtukufu (a.s), dirisha linalo wapa mikono watu wanaokuja kufanya ziara na kumuomba Mwenyezi Mungu akidhi haja zao kwa baraka za mwezi wa familia (Abulfadhil Abbasi (a.s).

Katika siku hisi, hasa (15 Machi 2016 m) uliwasili msafara wa wapenzi wa Abbasi (a.s) wakiwa wamebeba dirisha jipya kutoka katika kiwanda cha Ataba tukufu (Saqaau/1) katika haram tukufu, kwa kutengeneza kwao watumishi wa Atabatu Abbasiyya wakaingia katika historia ya kutengeneza dirisha la kwanza kwa mikono yao wenyewe..

Msafara huo ulikua na maeflu ya mazuwaru na wageni kutoka ndani na nje ya mji wa Sayyid Shuhadaau (a.s) Karbala takasifu wakiwemo viongozi wa dini, tamaduni, maafisa usalama, viongozi wa kikabila na vikundi (mawaakibu) za Husseiniyya.

Kituo cha kwanza cha msafara huo kilikua ni kiwanda cha Atabatu Abbasiyya tukufu cha kutengeneza madirisha ya kuweka katika makaburi ya Ataba na mazaru (maimamu na mawalii) kilicho tengeneza dirisha hilo, kisha wakaondoka na kuelekea katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu ya imamu Hussein na ndugu yake Abbulfadhil Abbasi (a.s).

Msafara huu ukatembea ukiwa umebeba sehemu za dirisha katika gari maalumu baada ya kufunikwa kwa utaalamu wa hali ya juu ukitanguliwa na wabeba bendera za Iraq pamoja na bendera zilizo andikwa (Ewe mwezi wa bani Hashim) huku wakiimba qaswida na mashairi yanayo dhuhirisha mapenzi na kufungamana kwao na huyu muheshimiwa mtukufu.

Wakapasua njia kuelekea katika kituo kilicho pangwa kuingilia ambapo ni mlango wa Bagdad, hapo walikusanyika watu wengi kuwapokea na wakaweka vizuizi barabarani na kuchinja wanyama njia nzima kuenelea hadi katika mlango wa Qibla wa imamu Hussein (a.s) kisha wakaelekea sehemu ya katikati ya haram mbili na katika mlango wa Qibla katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kuliwa kundi kubwa la watu wanao subiri kuwapokea na kutabaruku kwa kuliangalia dirisha la Abulfadhil Abbasi (a.s).

Sherehe za kiimani na kimapenzi zilizo kuwepo katika mji wa Karbala siku hizo za kuwekwa dirisha jipya katika kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) zilishuhudia kuongezeka kwa watu wanaokuja kufanya ziara kwa makumi ya maelfu na uhudhuriaji mkubwa wa viongozi wa kikabila wa mji wa Karbala mtukufu ambao walikua na nafasi muhimu katika hafla hizo kama walivyo kua babu zao katika miaka ya sitini ya karne iliyo pita wakati lilipo pokelewa dirisha la zamani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: