Atabatu Abbasiyya tukufu yafanikisha miradi ya ujenzi na utoaji wa huduma zaidi ya (150) kwa dola bilioni moja ndani ya miaka (13)!!

Maoni katika picha
Wakili wa Marjaa dini mkuu muheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi (d.i) ametangaza matumizi ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika kufanikisha miradi ya utoaji huduma na ujenzi mkubwa wakati na mdogo, aliyasema hayo katika hotuba yake aliyo ongea jana Juma Mosi katika uzinduzi wa mradi wa upanuzi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika upande wa upauaji, nao ni miongoni mwa miradi muhimu ya kiujenzi iliyo tekelezwa chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia shirika la Aridhi tukufu linalo milikiwa na wahandisi wa kiiraq, na kufanya haram ifikie uwezo wa kuingiza hadi watu (mazuwaru) elfu ishirini (20) ukiongeza na wahudumu wa haram.

Tangazo hili ni la aina yake, kiongozi wa kisheria katika Atabatu abbasiyya tukufu alisema kua: “Toka tupewe jukumu la kuitumikia Atabatu Abbasiyya katika mwaka wa (2003 m), katika kipindi cha miaka (13) kati ya (01/01/2004 hadi 01/01/2017) tumefanikisha zaidi ya miradi (150) ya ujenzi na ya utoaji wa huduma kwa dola bilioni moja tu”.

Akaongeza kusema kua: “Hii inamanisha kua matumizi ya utekelezaji wa miradi tukigawa kwa wastani wa kila mwaka itakua sawa na dola milioni (76) kwa mwaka”!!.

Pia Sayyid Swafi siku za nyuma, aliwahi kuuambia mtandao wa Alkafee wa kimataifa idara ya habari katika ofisi ya intanet (enternet) kua: “Matumizi hayo yanahusisha pia gharama za kiutendaji kama vile (mishahara, ugeni, matengenezo na mengineyo) na vyanzo vya mapato ya Ataba tukufu ni miradi ya kiuzalishaji ya Ataba na ruzuku tunayopata kutoka wakfu shia na sadaka zinazo patikana katika dirisha la Abulfadhil Abbasi (a.s) na zawadi pamoja na nadhiri”.

Marjaa dini mkuu katika hotuba ya Ijumaa ya mwisho (18 Jamadil Aakhira 1438 h) sawa na (17 Machi 2017 m) kupitia wakili wake Sayyid Ahmad Swafi (d.i) alikua amegusia mapungufu ya idara za serikali, na akasisitiza kua ni amana ambayo lazima wahusika waitekeleze, alisema kua: “Amana –ndugu zangu- ni katika mambo muhimu, anaye beba amana lazima awajibike, wakati mwingine unaweza kusema: mimi siwezi kutekeleza amana!! Mwenyezi Mungu atakulipa kheri, ondoka! Aje katika nafasi hiyo mtu anaye weza kutekeleza amana”.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Jumla ya miradi mikubwa iliyo tekelezwa na wataalamu wa kitengo chetu au waliyo isimamia baada ya kuwapa jukumu la utekelezaji moja ya shirika za kiiraq au kutekelezwa na kitengo kingine, miradi iliyo kamilika, midogo ya kati na mikubwa hatuwezi kuitaja yote, kwa haraka haraka ilikua kama ifuatayo:

Kusanifu na kutengeneza dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na kukarabati na kuweka dhahabu katika minara ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mradi wa upanuzi wa Atabatu Abbasiyya tukufu hadi kufikia mita za mraba elfu (30).

Upanuzi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika upande wa upauaji wa uanja wa haram tukufu.

Kusanifu na kujenga hospitali ya rufaa Alkafeel katika mji wa Karbala.

Kusanifu na kujenga hospitali ya rufaa Alkafeel katika mkoa wa Baabil (Ujenzi upo katika hatua za mwanzo na umesimama kwa sababu ya kukosekana pesa).

Mradi wa kujenga baadhi za sehemu katika ghorofa ya pili ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Majengo ya Abbasi (a.s) kwa ajili ya makazi, yenye kujumuisha nyumba (829) pamoja na shule, maduka, zahanati, majengo ya chini na barabara.

Mradi wa Gereji (Garage) ya Alkafeel.

Mradi wa kuendeleza (kupanua) jengo la maqaamu ya imamu Mahadi (a.f).

Mradi wa majengo ya kutoa huduma za Atabatu Abbasiyya tukufu katika barabara ya Najafu – Karbala.

Kuimarisha na kurejea kuweka dhahabu katika nguzo za jengo tukufu la haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mradi wa kiwanda cha usindikaji.

Jengo la wageni la imamu Haad (a.s).

Jengo la kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s) kwa ajili ya harakati za wanawake.

Mradi wa majengo ya viwanda na magodauni (Saqaau/2).

Mradi wa ukarabati wa kubba tukufu.

Mradi wa kuimarisha na kukarabati kuta na sakafu ya sardabu (tabaka la chini) la kaburi ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mradi wa kuanzisha jengo la kituo cha afya katika barabara ya Baabil – Karbala.

Mradi wa kuanzisha jengo la vyoo karibu na mlango wa kiganja cha mkono.

Mradi wa kutindua sakafu ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuiimarisha kwa cement.

Mradi wa kituo cha Atabatu Abbasiyya tukufu cha utunzaji wa maji na usafishaji wake.

Mradi wa kutengeneza barafu.

Kuanzisha kituo cha kebo za umeme katika eneo la katikati ya haram mbili.

Kujenga sehemu ya kuchukulia udhu na matenki ya maji ya kunywa katika barabara ya Abbasi (a.s).

Mradi wa majengo ya godauni na viwanda Saqaau/1.

Mradi wa umwagaji wa taka.

Majaribio ya kihandisi.

Mradi wa jiko la nje la watu wanaokuja kufanya ziara.

Kujenga ukumbi wa imamu Hassan (a.s) kwa ajili ya mikutano na nadwa.

Mradi wa viwanda na magodauni Saqaau/3.

Kiwanda cha kuzalisha cement.

Mradi wa vituo vya afya.

Mradi wa uhakiki wa kihandisi wa kielektronik katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mradi wa magodauni ya miswala.

Kiwanda cha kufyatua matofali.

Kukarabati na kuupendezesha ukuta wa nje wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kuanzisha kiwanda cha ukataji.

Mradi wa kunywesha maji wa kihuduma.

Majengo ya vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mradi wa kituo maalumu cha umeme katika majengo ya makazi ya Alkafeel.

Kituo cha kitamaduni na kiutumishi cha Atabatu Abbasiyya tukufu (majengo ya kwanza).

Majengo ya godauni na kituo cha ubora.

Mradi wa upanuzi wa maqaamu ya imamu Mahadi (a.f).

Majengo ya uwalimu na ufundishaji/2.

Idara ya magodauni (sehemu ya kwanza/ Alwafaau).

Majengo ya viwanda na godauni katika barabara ya Najafu – Karbala.

Sehemu ya pili katika mradi wa godauni za Ataba tukufu.

Mradi wa matangazo ya moja kwa moja (SNG).

Maahadi Alkafeel kwa wenye mahitaji maalumu.

Maahadi Alkafeel ya kutoa elimu na kuendeleza vipaji.

Kituo cha Alkafeel cha uchapishaji.

Maahadi ya Qur’an tukufu (inahusika na mambo ya maarifa ya Qur’an).

Kituo cha kiislamu cha masomo ya kimkakati.

Mji wa mazuwaru (watu wanaokuja kufanya ziara) katika barabara ya Najafu.

Kusanifu na kuanzisha Darul Kafeel ya uchapishaji na usambazaji.

Mradi wa maktaba na Darul Makhtutwati ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kuanzisha kituo cha barakaat cha Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya ufugaji wa kondoo.

Mashamba ya Khairaat Abulfadhil Abbasi (a.s).

Vitalu vya Atabatu Abbasiyya tukufu vya maua, asali na mimea.

Kiwanda cha Juud kinacho tengeneza pembejeo za kilimo.

Kiwanda cha A’alaaf Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mgahawa (mudhifu) wa Abulfadhil Abbasi (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mradi wa upanuzi wa milango ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mradi wa kituo cha mawasiliano na uangalizi na vituo vya ukaguzi.

Mradi wa kujenga mnara wa saa ya Atabatu Abbasiyya tukufu na kununua saa mpya.

Mradi wa kuweka mtandao wa mawasiliano katika majengo ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mradi wa kituo cha umeme cha Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mradi wa Saaqi wa kilimo cha tente ambazo ni nadra (chache sokoni).

Kiwanda cha usafishaji na vifaa vya kikemia.

Napenda kusema mifano michache katika mafanikio ya Atabatu Abbasiyya tukufu ambayo miradi yake inategemea akili za wairaq kwa asilimia kubwa, na wameonyesha mafanikio:

 1. Ujenzi (kama vile miradi ya ukarabati na upanuzi).
 2. Huduma (mfano ujenzi wa majengo ya kutoa huduma na kupokea mazuwaru na kupanda maua na mitu barabarani).
 3. Makazi (mfano nyumba za Abbasi (a.s) za makazi ya watumishi wa Ataba na majengo ya Barakaat Alkafeel ya makazi yakiwa ni mradi wa kiuchumi).
 4. Tiba (mfano hospitali ya rufaa Alkafeel ya Karbala, na hospitali ya rufaa ya Alkafeel –ambayo ujenzi wake umesimama kutokana na kusimama kwa ufadhili wa serikali- katika mji wa Baabil, miradi hii ya hospitali inalenga kuwahudumia wananchi, na inatoa sehemu ya tiba kwa wana jihadi bure, pia imeokoa makumi ya mamilioni ya dola za raia zilizo kua zikitumika kwa ajili ya kufata matibabu nje ya Iraq).
 5. Uchumi (miradi ya mashirika ya kiuchumi ambayo pato lake linatumika katika kuwahudumia mazuwaru na wakazi).
 6. Viwanda (vimesaidia kupunguza tatizo la baadhi ya mahitaji ya wakazi).
 7. Kilimo (mashamba ya mazao, mashamba ya nyuki, mabwawa ya samaki, na ufugaji wa mbuzi na kondoo).
 8. Tamaduni (ufunguzi wa maktaba, vituo vya utunzi na uhakiki wa kielimu, vituo vya turathi na mazingira, vituo vya kulea watoto wa kike na wakina mama).
 9. Habari (kuanzisha majarida, machapisho mbabali mbali na redio maalumu ya wanawake na watoto na kituo cha kurusha matangazo ya moja kwa moja).
 10. Usalama (mitambo ya uchunguzi ya video, mitambo ya mawasiliano na mitambo ya kugundua vilipuzi).
 11. Elimu (kuanzisha vituo vya utafiti na majarida ya kielimu, kuanzisha chuo na shule za watoto).
 12. Jeshi (kuanzisha kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji ambacho kimepata mafanikio makubwa katika vita, na Ataba imejitahidi kutekeleza amri ya Marjaa ya kutoa msaada kwa vikosi vya jeshi la Iraq, ili kuhakikisha havizaliwi vikundi vya magaidi).

Hakika mambo yapo mengi muda hautoshi kuzungumza yote..
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: