Zainabiyya za maelekezo ya kidini zahuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s)..

Maoni katika picha
Zainabiyya za kitengo cha maelekezo ya kidini upande wa wanawake chini ya kitengo cha habari na utamadumi katika Atabatu Abbasiyya tukufu mwaka wa tatu mfululizo wanahuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa kiigizo chema cha wanawake wa ulimwenguni bibi Fatuma Zaharaa (a.s).

Imefanyika hafla kabwa katika ukumbi wa imamu Hassan (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu na kuhudhuriwa na watumishi wa idara hiyo pamoja na wageni kutoka katika Ataba zingine na shule za wanawake zilizo chini ya Atabatu Abbasiyya katika mikoa ya Iraq.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikafuatia hotuba iliyo tolewa na mmoja wa watumishi wa idara, iliyo kua na anuani isemayo (Zaharaa (a.s) na muitikio katika mihrabu ya ibada).

Baada ya hotuba hiyo wanafunzi wa shule ya Fadak Zaharaa (a.s) walisoma qaswida na tenzi kuhusiana na mnasaba huu, pia wakafanya igizo kuhusu kisa cha kuolewa kwa bibi Fatuma (a.s) na Amirulmu-uminina Ali bun Abuutwalib (a.s), halafu ikaonyeshwa filamu inayo elezea ushujaa wa hashdi sha’abi na nafasi ya wanawake katika kuwasaidia.

Hafla ilikhitimishwa kwa kutoa zawadi kwa washindi wa mashindano yaliyo fanyika siku za nyuma pamoja na kuwapa zawadi waandalizi wa hafla hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: