Kamati imeweka taratibu na kanuni zifuatazo:-
- 1- Kisa kiandikwe kwa kufuata misingi ya kielimu na kimaadili.
- 2- Kisa kielezee ujasiri wa jeshi la Iraq na Hashdi Sha’abi kwa picha ya jumla (bila kumlenga mtu) katika kulinda nchi, maeneo matukufu, misingi ya kibinadamu na kimazingira.
- 3- Kisiwe kimesha wahi kutolewa, imma kwenye kitabu au mitandaoni au kimesha wahi kutolewa katika mashindano mengine.
- 4- Kiandikwe na kuhifadhiwa katika CD kwa program ya word na kiwasilishwe katika kitengo cha Habari na Utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na wasifu (CV) wa muandishi, au tuma kwenye email ifuatayo, (info@holyfatwa.com).
- 5- Mwisho wa kupokea ni 05/05/ 2017 m.
- 6- Nakala tano zitakazo shinda zitachapishwa kwa gharama ya Atabatu Abbasiyya pamoja na kutolewa zawadi maalumu kwa wahusika.
Kuna zawadi tano zimeandaliwa kwa visa vitano vitakavyo shinda, kila kimoja kitapewa laki mbili (200,000) dinari za Iraq.