Kamati imeweka kanuni na taratibu zifuatazo:-
- 1- Fikra ya filamu iendane na mtazamo wa kongamano.
- 2- Filamu ionyeshe ushujaa na ujasiri wa jeshi la Iraq na Hashdi Sha’abi kwa ujumla (sio kumlenga mtu) katika kulinda nchi, misingi ya kibinadamu, mazingira na maeneo matukufu.
- 3- Filamu isiwe imesha wahi kuonyeshwa katika vyombo vya habari au mitandao ya kijamii au katika maonyesho mengine.
- 4- Filamu itakayo shiriki ihifadhiwe katika CD na iwasilishwe katika kitengo cha Habari na Utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, ikiambatana na wasifu (CV) ya muandaaji, au tuma katika email ifuatayo (info@holyfatwa.com).
- 5- Mwisho wa kupokea filamu hizo ni 05/05/2017 m.
- 6- Filamu isiwe chini ya dakika moja na zisizidi dakika ishirini (20).
- 7- Aina ya filamu iwe (HD au avi).