Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kinaendelea kuitikia wito wa Marjaa dini mkuu kwa kujitolea roho na damu zao, Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya Juma Mosi ilimsindikiza shahidi miongoni mwa wapiganaji wake, naye ni (Shahidi Imadu Jawaad Hassum A’amiriy) aliye pata shahada katika vita ya kukomboa mji wa Badushi kutoka mikononi mwa magaidi, chini ya oporeshen ya tunakuja ewe Nainawa –upande wa kulia- (wa mji wa Mosul) akapanda meli ya mashahidi walio jitolea damu zao takasifu kwa ajili ya kulinda nchi na maeneo matukufu.
Alifanyiwa ziara na dua katika uwanja wa haram ya Abbasi takasifu na kuhudhuriwa na watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kundi la waumini kisha mwili wake ukapelekwa katika malalo ya Sayyid Shuhadaau imamu Hussein (a.s) kwa kupitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.
Shahidi A’amiriy ni miongoni mwa wakazi wa Karbala, alikua miongoni mwa watu wa kwanza kuitikia wito wa Marjaa dini mkuu, ameshiriki katika vita nyingi hadi kupata utukufu wa shahada katika vita hii ya kukomboa mji wa Mosul, Mwenyezi Mungu amrehemu na kumuweka mahala pema peponi.
Kumbuka kua kikosi cha Abbasi na kikosi cha 36/ cha jeshi la Iraq, walifanikiwa kukomboa mji wa Badushi baada ya vita kali, waliyo onyesha ushujaa na ujasiri wa hali ya juu, na wakatoa somo kali kwa Daesh ambalo hawata lisahau milele, vita vya kukomboa mji huo vilipelekea vifo vya makumi ya magaidi ya Daesh..
Wapiganaji wetu sasa hivi wanafanya kazi ya kusafisha mji kwa kutegua mabomu yaliyo tegwa aridhini ndani ya mji huo.