Maahadi ya Qur’an tukufu yafanya mashindano ya Zaharaa (a.s) ya Qur’an kwa wanafunzi wa shule za mkoa wa Bagdad..

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’an tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya tawi la Bagdad imefanya mashindano ya Qur’an kwa wanafunzi wa shule za upili (sekondari) katika ofisi zake zilizopo kitongoji cha Sha’abu, mashindano hayo yamedumu siku mbili na kushiriki makumi ya wanafunzi, yanalenga kujenga mapenzi ya Qur’an katika roho za washiriki na wahudhuriaji.

Pia yanasaidia kutambua vipaji vya Qur’an kwa vijana wetu na kuvilea, na kutengeneza jopo la wasomi wa Qur’an tukufu watakao saidia kusambaza nuru yake katika jamii, mashindano yaliangalia vitu mbalimbali, kama vile: hukumu za usomaji, sauti na naghma (mvumo wa sauti), kulikua na ushindani mkubwa baina ya washiriki, pia yalipata mahudhurio makubwa ya walimu na viongozi mbalimbali, pamoja na wadau wakubwa wa Qur’an katika mji mkuu wa Bagdad.

Mwishoni mwa mashindano ziligawiwa zawadi kwa washindi watatu wa mwanzo, na wakapewa zawadi pia kamati ya majaji walio simamia mashindano na walimu walio toa mchango mkubwa katika kufanikisha mashindano haya.

Tunapenda kusema kua mashindano haya ni hatua kubwa inayo wahamasisha vijana kujikita katika Qur’an na kufikia maendelea makubwa, yanafanikishwa kutokana na juhudi kubwa za walimu na viongozi wa Maahadi ya Qur’an tukufu za kuandaa mazingira mazuri ya kufanyika kwa mashindano haya kwa ufanisi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: