Taarifa kutoka katika kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji zinasema kua, majemedari hao; jana Juma Nne (22 Jamadil Aakhira 1438 h) sawa na (21 Machi 2017 m) wamefanikiwa kuua madaesh (77) walio jaribu kuwashambulia wao pamoja na jeshi la serikali katika milima ya Badushi.
Habari ikafafanua kua: “Wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) walifanikiwa haraka kuzuia shambulio hilo na kuwaua magaidi wote waliokuja kuwashambulia”.
Habari zingine zinasema kua wapiganaji wa kikosi hicho waligundua sehemu iliyo kua inatumika kutengenezea vilipuzi na kuviweka katika magari kwa ajili ya kwenda kulipua maeneo mbalimbali ndani ya upande wa kulia wa mji wa Mosul, pia wameona ramani inayo onyesha namna ya kulibua majengo, vilevile wameteka magari mengi ya daesh yaliyojaa vilipuzi.
Fahamu kua kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji wamekamilisha maandalizi yote ya kuvamia kijiji cha Bubu Sham magharibi ya Mosul na kufika hadi katika mto wa Dujla.