Kwa namba: Haya ndio yaliyo fanikishwa na wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) katika vita ya kukomboa upande wa kulia wa mji wa Mosul..

Maoni katika picha
Viongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji asubuhi ya siku ya Alkhamisi ya tarehe (24 Jamadil Aakhira 1438 h) sawa na (23 Machi 2017 m) walifanya mkutano na waandishi wa habari katika makao makuu yao, na kuhudhuriwa na waandishi wa vyombo vya aina mbalimbali, luninga (tv), redio na magazeti, wakaelezea mafanikio waliyo pata katika oporesheni ya (tunakuja ewe Nainawa) ya kukomboa upande wa kulia wa mji wa Mosul.

Kiongozi mkuu wa kikosi Ustadh Maitham Zaidi alibainisha kua: “Hakika kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kimeshiriki katika vita ya kukomboa upande wa kulia wa mji wa Mosul, tukiwa kama Hashdi Sha’abi tulio ungwa mkono na vikosi vingine, kutokana na maelekozo ya kamanda wa vikosi vya wapiganaji pamoja na kamanda wa vikosi vya muungano, Alhamdu lillahi; sisi tulipata utukufu wa kushirikiana na jeshi la Iraq na tukafanywa kua wawakilishi rasmi wa Hashdi Sha’abi katika vita hii tukufu.

Akabainisha kua: “Tulikua na vituo vitatu upande wa magharibi ya mji, kikosi cha 36/ cha jeshi la Iraq kilishirikiana nasi, pia kikosi cha 71/ kikaungana nasi baada ya siku thelathini toka kuanza kwa mapigano, matokeo ya vita yalikua kama ifuatavyo:

  • 1- Tumeau zaidi ya Madaesh (420) katika vita hii, na watu muhimu tulio waua ni; Mkuu wa upelelezi wa Daesh Aadil Dhanuun Ismaeel, mkuu wa mawasiliano Ahmad Abuu Maaliki, mkuu wa idara Abuu Anasi, msaidizi wa mkuu wa idara Muhammad Ali Abuu Mustwafa, bwana jela mkuu Abdullahi Ahmad Jaasim, mkuu wa taarifa Salam Abuu Swakar, na tumekabidhi mateka mia moja walio kiri makosa yao, wakiwemo wawili wamekiri kushiriki katika unyama uliofanywa katika jela ya Badushi.
  • 2- Tumekomboa zaidi ya kilometa (273) za mraba kwa kushirikiana na kikosi cha 36/ cha jeshi la Iraq, miongoni mwa maeneo tuliyo komboa ni; milima ya Nuwikitu, kitongoji cha Tal-kaisum, kitongoji cha Sahaji, milima ya Atwishana, makamanda wa kikosi cha muungano walituthibitishia kua kukombolewa kwa maeneo hayo kunarahisisha kukombolewa kwa upande wa kulia wote wa mji wa Mosul, ukizingatia kua sehemu hizo zinazunguka maeneo muhimu ya mji, kisha tulikomboa kitongoji cha Thalja na tukadhibiti njia ya mwisho, ambayo ni njia ya Batushi na tukapanda katika milima ya Badushi na kukomboa kiwanda cha cement kisha tukakomboa hodhi la Badushi halafu tukafanikiwa kukomboa mji wote wa Badushi pamoja na vijiji vya Hayya Swabihi na vinginevyo, pia tulidhibiti njia kuu inayo unganisha baina ya Tal-afar Mahlabiyya na upande wa kulia wa Mosul.
  • 3- Tumepigana vita ya aina tatu kwa wakati mmoja, kwanza vita katika maeneo ya wazi, pili; katika maeneo ya milima, kila mtu anajua ugumu wa vita vya milimani, wapiganaji wote wa adui tulio pambana nao katika milima ya Badushi walikua ni wageni, huenda kilikua kikosi chao maalumu, na aina ya tatu ni vita ya ndani ya nyumba za raia na mitaani, tuliwapiga wakiwa wamejificha vyumbani, tuna mshukuru Mwenyezi Mungu katika aina zote hizo tatu tumemshinda adui na kumpa hasara kubwa huku sisi tukipata hasara ndogo sana”.

Akaongeza kua: “Tunashukuru watu wote wanao tusaidia wakitanguliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kama sio wao kusingekua na kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s), wamekua wakitoa msaada mkubwa sana kwetu, hususan kutujenga kisaikolojia pale anapo kuja kututembelea wakili wa Marjaa dini mkuu na kiongozi wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyidi Ahmad Swafi (d.i) na viongozi wengine wa Ataba kwa ujumla, bila kusahau mchango mkubwa wa kamanda mkuu wa vikosi vya wapiganaji anao toa kwetu daima, amekua karibu sana na sisi katika kutekeleza wajibu tulio pewa, pia tunaishukuru sana wizara ya ulinzi, waziri wa ulinzi ametoa ushirikiano mkubwa na ametutembelea mara kwa mara, hali kadhalika tunawashukuru Hashdi Sha’abi wametoa ushirikiano mkubwa sana katika vita hii.

Akafafanua: “Leo tunatangaza kumalizika kwa vita katika upande huu, wanajeshi wetu wataendelea kulinda usalama hadi tukomboe mji wote wa Mosul, tupo tayari kupokea agizo lolote kutoka kwa viongozi wa kuu wa vita hii, baadhi ya wapiganaji wetu wameenda kujiandaa kwa ajili ya vita ya Tal-afar kama tulivyo pewa taarifa kua tutakua moja ya majeshi yatakayo shiriki huko”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: