Kamati ya maandalizi ya kongamano la fatwa tukufu ya kujilinda yatangaza mashindano ya makala bora na yawataka wana habari washiriki..

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la fatwa tukufu ya kujilinda yawaomba waandishi wa habari washiriki katika shindano la Makala bora kuhusu fatwa ya kujilinda na ushujaa wa Hashdi Sha’abi, mashindano hayo yatafanyika katika kongamano litakalo simamiwa na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, ikiwa ni sehemu ya kuhuisha kumbukumbu ya kutolewa kwa fatwa hiyo, chini ya kauli mbiu isemayo: (Fatwa.. ni msingi wa ushindi na miski ya shahada) na wametangaza kanuni na mashariti ya kushiriki katika mashindano hayo kama ifuatavyo:

  • 1- Mshiriki ana haki ya kuchagua namna ya uandishi wa jarida (Makala) anao ona unafaa (Makala ya maoni, Makala ya utambulisho au Makala ya kuelezea) kwa kuchagua mada inayo endana na fatwa ya kujilinda au Hashdi Sha’abi.
  • 2- Makala izungumzie ushujaa wa Hashdi Sha’abi kwa ujumla bila kumlenga mtu maalumu, katika kulinda nchi, ubinadamu wanao onyesha na kulinda mazingira.
  • 3- Makala iandikwe kwa lugha sahihi ya kiarabu, na ikamilishe sharti za Makala –uzuri, muonekano, ufasaha wa lugha, uwiano wa maneno na ufupisho-.
  • 4- Makala isiwe imesha wahi kutolewa na watu wengine, na iwe imeandikwa na muhusika sio ya kupewa au kukopi kazi ya mtu mwingine.
  • 5- Isiwe chini ya maneno (300) na yasizidi (700).
  • 6- Isiashirie ubaguzi au kushambulia au mambo yasiyo kua ya kimaadili.
  • 7- Hairuhusiwi mshiriki kuandika Makala zaidi ya moja.
  • 8- Kamati ya maandalizi inahaki ya kuto onyesha Makala yeyote itakayo kosa sifa tulizo taja hapo juu.
  • 9- Kamati ya majaji inahaki ya kuzuia zawadi ya mshiriki yeyote watakapo kungua dosari kuhusu mshiriki huyo.
  • 10- Hairuhusiwi kwa mshiriki kuzalisha Makala yake kwa wingi na kuisambaza hilo litakua ni jukumu la kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • 11- Makala ziandikwe katika program ya (ward) na zihifadhiwe kwenye (CD) na kuwasilishwa katika ofisi za kitengo cha habari na utamaduni pamoja na wasifu (CV) wa muandishi, au zitumwe kwenye anuani hii (info@holyfatwa.com).
  • 12- Mwisho wa kupokea ni 05-05-2017 miladia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: