Atabatu Abbasiyya tukufu yawapongeza wahitimu wapya wa kitengo cha maarifa ya Qur’an katika chuo kikuu cha Mustanswiriyya..

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya hafla ya kuwapongeza wahitimu wa kitivo cha Tarbiyya katika chuo kikuu cha Mustanswiriyya awamu ya nne, hafla hiyo imefanyika asubuhi ya siku ya Juma Mosi (26 Jamadil Aakhira 1438 h) sawa na (25 Machi 2017 m) na hii ni miongoni mwa program za kijana mzalendo wa Alkafeel, hafla imefanywa ndani ya ukumbi wa imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, hafla hii ni miongoni mwa njia za kuwahimiza na kuwataka waongeze juhudi katika kuitumikia Qur’an tukufu.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fatha maalumu kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukaimbwa mwimbo wa taifa na mwimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kisha ukafuatia ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na Shekh Harith Daahi, miongoni mwa aliyo sema ni: “Tunakukaribisheni enyi wanafunzi katika sehemu hii tukufu, makao makuu ya shahada chini ya kivuli cha kipenzi wetu Abulfadhil Abbasi (a.s), hakika mtume (s.a.w.w) katika hadithi yake mutawatiri ametuamrisha kushikamana na kamba imara, ambayo ni Qur’an na kizazi chake, kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu katika kipindi cha miaka mliyo soma mmetambua baadhi ya maarifa ya Qur’an na mmekua miongoni mwa wenye kubeba ujumbe huu wa milele, madamu tayali mmepata hii lulu muhimu jitahidini kushikamana na kizazi kitakasifu, huu ndio wasia wa mtume (s..a.w.w) mwatakiwa kuuzingatia”.

Kisha ukafuatia ujumbe wa chuo kikuu cha Mustanswiriyya uliosomwa na dokta Muhandi Abdali ulio sema kua: “Tupo kwa mtu mtukufu aliye itambua dunia vilivyo, tulifikiri tukaona wanafunzi wa chuo kikuu cha Mustanswiriyya kitengo cha maarifa ya Qur’an tukufu hafla ya kumaliza masomo yenu tuifanyie sehemu hii tukufu, kwa mtu mwenye sifa ya utekelezaji, ni upi huo utekelezaji? Ni ule alio ufundisha Abbasi (a.s) namna gani uwe mtekelezaji, nyoyo zenu ziwe na utulivu kwani nyie ni wanafunzi wa Qur’an, na mpo mbele ya mtu aliye ijua Qur’an na akaifundisha kwa vitendo, Qur’an imeandikwa na Abbasi analiishi kwa kufuata Qur’an, mwisho tunaishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mapokezi mazuri na kwa misaada yake endelevu kwa wanafunzi wa vyuo”.

Baada ya hapo kikatolewa kisa cha (Kumbukeni) ambacho kilielezea maisha ya wanafunzi wa vyuo na mazingira magumu wanayo pitia katika kipindi hiki cha wimbi la ugaidi, lakini wanaendelea kua na subira na kujitahidi katika masomo yao.

Kisha ulifuata ujumbe wa wahitimu ulio wasilishwa na Hussein Zaidi, aliwashukuru walimu kwa juhudi zao kubwa za kuwafundisha na wakaishukuru Atabatu Abbasiyya kwa msaada endelevu kwao, hafla ilihitimishwa kwa picha ya pamoja ya wahitimu na walimu wao na chuo kikuu cha Mustanswiriyya kiliwapa vidani Atabatu Abbasiyya tukufu, pia hafla ilipambwa kwa beti za mashairi ya kuwasifu Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: