Kwa ushiriki wa kimataifa: Hafla ya Qur’an yafanyika ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu..

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratuba za kongamano la kwanza la kitamaduni na kimataifa Ruhu Nubuwa linalo simamiwa na idara ya shule za Alkafeel za wasichana, chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu likiwa na kauli mbiu isemeyo: (Zaharaa –a.s- ni hazina ya elimu na kilele cha hekima).

Jioni ya siku ya Ijumaa (25 Jamadil Aakhira 1438 h) sawa na (24 Machi 2017 m) ilifanyika hafla ya Qur’an katika Sardabu ya imamu Mussa Al-kaadhim (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha akazungumza kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu (d.i), alisisitiza umuhimu wa kushikamana na kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu na kutekeleza mafundisho yake, pia alisisitiza umuhimu wa kusoma Qur’an kwa ufasaha na kutengeneza kizazi cha wasichana ambao ni wasomi wa Qur’an tukufu.

Kisha lilionyeshwa igizo lililo andaliwa na Maahadi ya Qur’an kitengo cha wanawake lenye anuani isemayo: (Roho yangu inatokana na nuru), lilihusu madhumuni ya aya isemayo: (Na huwalisha chakuka, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa).

Halafu ilisomwa Qur’an tukufu na mabinti kutoka nchi mbalimbali, washiriki walikua ni kutoka Iraq, Iran na Lebanon, wakamalizia kwa kisomo cha wanafunzi wa madrasat Fadak Zaharaa (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: