Kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili chafanya semina ya utambuzi wa vilipuzi na namna ya kuvitegua..

Sehemu ya semina
Idara ya utambuzi wa vilipuzi chini ya kitengo cha; katikati ya haramu mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimefanya semina ya utambuzi wa vilipuzi, na kuhudhuriwa na watumishi wa kitengo cha kulinda nidhamu cha Ataba mbili tukufu pamoja wa watumishi wa idara.

Wawezeshaji (wakufunzi) wa semina hii ni wataalamu wa kijeshi kutoka Bagdad, inalenga kuongeza viwango vya watumishi katika kutambua vilipuzi na mabomu na namna ya uteguzi wake au kuzuia yasitokee madhara kwa kutumia njia za kisasa, hii ni kutokana na umuhimu wa kazi yao ambayo ni kuhakikisha usalama kwa mazuwaru watukufu (watu wanaokuja kufanya ziara), pia wamefundishwa utoaji wa huduma ya kwanza pindi inapo tokea kulipuka bomu moja kwa moja.

Kumbuka kua Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kwa ajili ya kuongeza uwezo wa watumishi wao hufanya semina za mara kwa mara, kila kitengo na fani yao, chini ya ukufunzi wao wenyewe au kwa kutumia wakufunzi kutoka nje ya Ataba mbili tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: