Wametaja mada zitakazo shindaniwa kuwa ni:-
Kwanza: Nafasi ya vyombo vya habari katika kuhuisha na kudumisha uzalendo kabla ya ukombozi na maada yake.
Pili: Mapambano ya vyombo vya habari dhidi ya taasisi za kitaifa na kimataifa zinazo unga mkono ugaidi pamoja na vyombo vya habari vya madaesh na wafuasi wao.
Tatu: Nafasi chanya ya vyombo vya habari kwa Ataba katika kufikisha fatwa tukufu kwa jamii ya kitaifa na kimataifa na kujibu upotoshaji na uzushi kuhusu swala hilo.
Nne: Kufanyiwa kazi usia na maelekezo ya Marjaa kwa wapiganaji ndani ya uwanja wa vita.
Tano: Matendo ya kibinadamu na kizalendo yanayo fanywa na wapiganaji katika vita ya ukombozi.
Sita: Athari chanya ya jamii na familia za wairaq katika kuwaandaa watu wake kukubali fatwa na kujitolea kwa ajili ya kukomboa nchi yao.
Saba: Undani wa kihistoria wa fatwa tukufu ya kujilinda, na athari yake katika kuamsha moyo wa Husseiniyya.
Nane: Juhudi za watu wa sekula katika kuthibitisha na kufundisha mambo yanayo tokea.
Tisa: Nafasi ya mitandao ya kijamii na athari yake katika kubainisha ubinadamu na uzalendo na kuwajibu waovu na wapotoshaji wa habari.
Sharti za ushiriki ni hizi zifuatazo:
- 1- Makala isiwe chini ya kurasa (20) na zisizidi (25).
- 2- Makala iandikwe kwa hati ya (simplified Arabic) ukubwa wa herufi uwe saizi (16).
- 3- Utafiti uendane na malengo ya kongamano na uwe ndani ya mada tajwa hapo juu.
- 4- Mwisho wa kupokea Makala zitakazo shindanishwa ni (05/05/2017 m).
- 5- Makala iandikwe na kuhifadhiwa katika (CD) Na iwasilishwe katika ofisi za kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu au itumwe katika barua pepe ifuatayo, (info@holyfatwa.com).