Baada ya kufunga kifaa cha kisasa na kimataifa katika tiba ya saratani, na kuwaandaa madktari na wauguzi kwa kuwapa semina ya namna ya kutumia kifaa hicho, idara ya hospitali ya rufaa Alkafeel iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, katika hatua ya mwanzo, wameanza kupokea wagonjwa wa saratani ya matiti kwa mara ya kwanza, wamefanikiwa kutibu wagonjwa kumi wa saratani hiyo imma kwa kukata titi (kwa wale ambao ugonjwa umefikia hatua mbaya zaidi) au kutibu kwa kutumia mionzi.
Akielezea huduma inayo tolewa na hospital ya rufaa ya Alkafeel Daktari Lithi Sharishiy alisema kua: “Katika siku za hivi karibuni hospitali ya rufaa Alkafee imefanikiwa kutibu wanawake kumi walio kua na tatizo la saratani ya matiti, kwa kutumia kifaa cha kisasa kabisa, ambacho kinatumika hapa Iraq kwa mara ya kwanza, chini ya madaktari mahiri.
Akafafanua kua: “Hakika vifaa vya mionzi ambavyo vina uwezo mkubwa wa kutibu maradhi ya saratani bila kuathiri sehemu za jirani na vilipo virusi vya saratani, vinatengenezwa na shirika moja tu duniani, na hospitali pekee inayo miliki kifaa hicho hapa Iraq ni hospitali yetu, Iraq imekua miongoni mwa nchi mia moja zinazo miliki kifaa hiki chenye uwezo wa kutubi saratani ya matiti bila upasuaji.
Kumbuka kua; Saratani ya matiti ni miongoni mwa maradhi hatari zaidi kwa wanawake katika zama hizi, inasababisha vifo kwa asilimia (18.2%) katika jumla ya wanawake wanao sumbuliwa na maradhi hayo, wanawake wenye umri mkubwa wapo katika hatari zaidi ya kupata maradhi hayo, idadi ya waathirika wa saratani ya matiti inakadiriwa kua (232,340) na idadi ya vifo vitokanavyo na saratani ya matiti inakadiriwa kua (39,320) kutokana na takwimu za shirika la saratani la kimarekani.
Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zinazo tolewa na hospitali tembelea tohgut yetu (www.kh.iq) au piga simu: (07602344444) au (07602329999).