Shirika la Usalama la Alkafeel latembelea nyumba ya wazee katika mji wa Najafu Ashrafu..

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba zake za kijamii, na kufatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s) pamoja na furaha waliyo nayo wairaq ya sikukuu ya mama, idara ya usalama ya shirika la Alkafeel ikiwakilishwa na kiongozi mkuu mtendaji, wamewatembelea wakina mama waliopo kwenye nyumba ya wazee katika mkoa wa Najafu Ashrafu, kupongeza juhudi zao na kuwapa zawadi, kuonyesha thamani ya nguvu zao walizo tumia katika kujenga familia na nchi wakati wa ujana wao.

Ustadh Muhandisi Aarif Bahaashi kiongozi mkuu mtendaji wa usalama katika shirika la Alkafeel amesema kua: “Idara ya utendaji ya shirika la usalama la Alkafeel katika kuhuisha kwake mazazi ya bibi Fatuma Zaharaa (a.s) ikifungamana na siku ya mama imewatembelea wakina bibi waliopo kwenye nyumba ya kutunza wazee katika mkoa wa Najafu Ashrafu, na kuwapa zawadi pamoja na kuwawezesha kuwasiliana na familia zao bure pia tutawapangia ziara ya kutembelea Ataba tukufu kwa gharama za shirika, na tuliuliza mahitaji yao na mahitaji ya wasimamizi wao, hakika wana ushirikiano mkubwa sana na wanawajali sana wasimamizi wao”.

Mkuu wa nyumba hiyo Ustadh Alaa Khuz-ali amesifu sana maamuzi ya shirika la usalama la Alkafeel kwa kuwatembelea na kuangalia mahitaji yao, ametuomba tuwasaidie simu kwani zitawarahisishia kuwasiliana na ndugu zao na kutuliza nafsi zao, pia amepongeza kuwawekea ratiba ya kutembelea Ataba tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: