Katibu mkuu wa mazaru za kishia atembelea banda la Atabatu Abbasiyya tukufu katika maonyesho ya vitabu na kimataifa huko Bagdad na asifia..

Maoni katika picha
Muheshimiwa shekh Sataar Jizani katibu mkuu wa mazaru za kishia nchini Iraq amesifu nafasi iliyo nayo Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta ya elimu na utamaduni ambayo inaonekana bayana kupitia maonyesho yake inayo fanya katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa yanayo endelea sasa hivi katika mji mkuu wa Bagdad.

Shekh Jizani alipo tembelea banda la Atabatu Abbasiyya tukufu ambapo kitengo cha Habari na Utamaduni na kitengo cha Maarifa ya kiislamu na kibinadamu wameshiriki katika maonyesho hayo, amesema kua; tuliyo yaona miongoni mwa vitabu na machapisho mbali mbali yana athari ya wazi juu ya kutoa elimu kuhusu uislamu halisi.

Shekh Jizani alisikiliza maelezo kutoka kwa wahudumu wa banda hilo, ambapo walielezea vitabu na machapisho waliyo nayo, ambapo yanagusa watu wa rika na tabaka zote, na jambo la pekee kwao ni kwamba vitabu vyote walivyo navyo ni zao la Ataba tukufu kuanzia uandishi hadi uchapaji.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki mara nyingi katika maonyesho ya kimataifa ya Bagdad, ambayo huzingatiwa kua maonyesho muhimu kwake, ikiwa ni pamoja na kushiriki katika maonyesho na makongamano yanayo fanyika ndani na nje ya Iraq, yanayo endana na mwenendo wa Ataba wa kusambaza fikra na mafundisho ya Ahlulbait (a.s), wawakilishi wake hupata mwitikio mkubwa kutoka kwa wadau wa maonyesho na hujitahidi kuongeza bidhaa mpya katika kila maonyesho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: