Ujenzi wa upanuzi wa Maqaamu ya imamu Al-muntadhir (a.f) waingia awamu ya pili..

Maoni katika picha
Baada ya kumaliza umwagaji zege awamu ya kwanza katika mradi wa upanuzi wa Maqaamu ya imamu Mahadi (a.f), jopo la mafundi na wahandisi chini ya usimamizi wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wameingia awamu ya pili ya ujenzi huo, hatua hii imetanguliwa na kazi nyingi za awali, kama vile kuandaa sakafu kwa kumwaka zege na kuweka nguzo za zege, ikiwa ni pamoja na nguzo za pembezoni mwa mto Husseiniyya, kwani upanuzi huu unahusisha kufunika mto na kusimamisha jengo juu yake.

Kwa mujibu wa rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh, ujenzi huu umehusisha kuweka daraja juu ya nguzo za zege ili baada yake iendelee hatua nyingine kutokana na ramani (mchoro) wa jengo, daraja zimefika (15) kila moja ina urefu wa mita (14) na uzito unakaribia tani (10) na unene wa sintimita (85) zimewekwa kwa kutumia vifaa vya kisasa vinavyo zifanya kua imara zaidi na kudumu kwa muda mrefu.

Akaongeza kusema kua: “ Sehemu hii ni ukumbi wa wanaume na inaukubwa wa mita za mraba (310) na sehemu nyingine ya watumishi wa Maqaamu yenye ukubwa wa mita za maraba (150), na sehemu iliyo baki itakua ya vyoo vya watumishi, kazi itagawika sehemu mbili kama ilivyo kua katika awamu ya kwanza, urefu wa sehemu hii unazidi mita (6)”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu ndio inayo fanya ujenzi na ukarabati wa Maqaamu ya imamu Mahadi (a.f) kuanzia Kubba, kumbi za haram, vyoo na sehehemu zingine, kwa kua sehemu ilipo Maqaamu hauwezi kufanya upanuzi katika pande zake tatu, hivyo upanuzi huu unafanywa upande wa mto wa Husseiniyya ambao ni upande wake wa magharibi katika eneo lenye ukubwa wa mita za mraba (1200) na unaingia katika Maqaamu kwa kutumia milango maalum.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: