Atabatu Abbasiyya tukufu yasimamia maonyesho ya kwanza ya uchoraji wa watoto katika mkoa wa Baabil..

Maoni katika picha
Chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kitengo cha habari na utamaduni; uongozi wa juu wa miradi ya Hilla mji wa imamu Hassan Mujtaba (a.s) asubuhi ya siku ya Juma Nne (29 Jamadil Aakhira 1438 h) sawa na (28 Machi 2017 m) wamesimamia maonyesho ya kwanza ya michoro ya watoto wa shule za msingi chini ya kauli mbiu isemayo (Kwanyoya langu la rangi ndio ushindi wangu) kwa kusaidiana na uongozi wa malezi na walimu wa mkoa wa Baabil.

Maonyesho haya yanayo fanyika katika ukumbi wa shule ya msingi binafsi Mazaya yamekuja wakati ambao jeshi letu na Hashdi Sha’abi wanapata ushindi mkubwa katika uwanja wa vita, picha zinazo shiriki katika maonyesho haya ni zile zinazo onyesha ushujaa na namna wanavyo jitolea wapiganaji wetu watukufu.

Maonyesho yalifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukaimbwa mwimbo wa taifa, kisha Ustadh Abduridhwa Mukhifu akawasilisha ujumbe wa uongozi mkuu wa miradi ya Hilla mji wa imamu Hassan Al-mujtaba (a.s) nao ndia waandalizi wa maonyesho haya, alisema kua: “Kwa ajili ya kuunga mkono mashujaa walio itikia wito wa Marjaa dini mkuu wa kuilinda aridhi ya Iraq na raia wake pamoja na maeneo matukufu, leo tunafanya maonyesho ya kwanza ya michoro ya watoto wa shule za msingi kwa kushirikiana na uongozi wa malezi na jopo la walimu wa Baabil”.

Akabainisha kua: “maonyesho haya zimeshiriki shule za msingi (26) za wavulana na wasichana kila shule imetoa kazi tano za kushiriki katika mashindano, hivyo jumla ya kazi zilizo shiriki ni (120), tumeunda jopo la majaji walio chagua jumla ya kazi (30) zitakazo shindanishwa katika maonyesho haya”.

Kisha baada ya hapo ulifuata ujumbe wa mkuu wa kituo cha malezi cha Baabil ulio wasilishwa na Ustadh Thaair Wahid ambaye ni mjumbe wa chama cha walimu katika mkoa wa Baabil, aliwashukuru waandaaji wa maonyesho haya, akaelezea umuhimu wa kufanyika kwa maonyesho ya aina hii kwa watoto yanaimarisha uzalendo wao, kisha washiriki walionyesha baadhi za kazi zao, baada ya hapo wahudhuriaji waote wakaelekea katika ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo, ambayo yalikua na picha nyingi zinazo onyesha ushujaa, ujasiri na ushindi wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi, mwisho zilitolewa zawadi kwa shule zilizo shiriki na kwa watoto waliofuzu katika mashindano ya maonyesho hayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: