Ofisi ya Mrjaa dini mkuu Muheshimiwa Ayatullahi Sayyid Ali Sistani (d.dh) imetangaza kua kesho siku ya Alkhamisi (30 Machi 2017 m) ni siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Rajabu Aswabu (1438 h) na leo siku ya Jumatando ndio siku ya mwisho ya mwezi wa Jamadil Aakhira.
Mwezi wa Rajabu ni mwezi wa Mwenyezi Mungu, ni miongoni mwa mwezi mitukufu, pia ndio mwezi aliozaliwa Amirulmu-uminina Ali bun Abuutwalib (a.s), unaitwa Aswabu kwa sababu Mwenyezi Mungu mtukufu humimina rehema kwa ummati Muhammad (s.a.w.w) uingiapo mwezi huu, nao ni mwezi wa kufanya Istighfaar, katika siku ya kwanza inasuniwa kufanya a’amaali nyingi miongoni mwake ni:
Kwanza: Kufunga, imepokwa kwamba Nabii Nuhu (a.s) alipanda Safina katika siku hiyo na akawaambia watu wake wafunge, na atakae funga siku hii atakua mbali na moto mwendo wa mwaka mmoja.
Pili: Kuoga.
Tatu: Kumzuru imamu Hussein (a.s) amepokea Sheskh kutoka kwa Bashiri Dahaan kutoka kwa Swaadiq (a.s) anasema: (Atakae mzuru Hussein bun Ali (a.s) siku ya kwanza ya mwezi wa Rajabu Mwenyezi Mungu atamsamehe kabisa).
Mwenyezi Mungu awakubalie waumini a’amaali zao na awape malipo makubwa, na awape baraka, kheri nyingi na rehema katika mwezi huu mtukufu, na wasitusahau katika dua zao.