Usiku wa Raghaaibu: Maana, Fadhila na A’amaali zake..

Maoni katika picha
Maana yake ni usiku wa kutoa sana, usiku huu mtukufu (Usiku wa Raghaaibu) una dalili inayo thibitisha ubora wake mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu, humpa thawabu nyingi sana atakae funga na akasimama usiku wake kwa kuswali na kusoma dua na kufanya ibada na matendo mema, katika usiku huu, watu walio funga na kufanya maghfira hupatiwa mahitaji yao, kwa sababu hiyo malaika wakauita usiku huu kua ni usiku wa Raghaaibu, nayo ni Alkhamisi ya kwanza ya mwezi wa Rajabu katika kila mwaka, mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) anasema (…Msighafirike katika usiku wa Ijumaa ya kwanza -ndani ya mwezi wa Rajabu- hakika usiku huo malaika wanauita kua ni usiku wa Raghaaibu, kwa sababu inapo fika theluthi ya usiku malaika wote wa mbinguni na aridhini hukusanyika katika Kaaba tukufu na pembezoni mwake kisha Mwenyezi Mungu huwaambia: Enyi Malaika wangu niombeni mtakacho, nao husema: Ewe Mola wetu shida yetu kwako uwasamehe waliofunga Rajabu. Mwenyezi Mungu huwaambia, nimesha wasamehe).

Usiku wa Raghaaibu una a’amaali nyingi, Mtume (s.a.w.w) anasema: (Mtu yeyote atakae funga Alkhamisi ya kwanza ya mwezi wa Rajabu kisha akaswali baina ya Isha na Atama (Maghribi) rakaa kumi na mbili, atakapo maliza aniswalie mara sabini, aseme: Allahumma swali alaa Muhammad wa ala aalihi, kisha asujudu na aseme akiwa katika sajda mara sabini, Subbuuhu Qudduusu Rabbul-malaaikatu wa rruuhu, kisha anainuka katika sajda na aseme: Rabbighfir warham wa tajaawaz Ammaata’alam innaka antal aliyyul a’adham, kisha anasujudu tena na anasoma kama alivyo sema mara ya kwanza, kisha amuombe Mwenyezi Mungu shida zake akiwa katika sijda atakidhiwa).

Kisha mtume (s.a.w.w) akasema: (Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu ipo katika milki yake, hataswali mja au umma swala hii ispokua atasamehewa dhambi zote hata kama zikiwa nyingi kama povu la bahari, na atapewa nafasi ya kuwaombea shifaa siku ya kiama watu mia saba katika familia yake walio kua wamehukumiwa kuingia motoni…).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: