Ujumbe wa siku ya kwanza ya wiki ya kitamaduni awamu ya nne Pakistani (Nasimu Karbala)..

Maoni katika picha
Mji mkuu wa Pakistani alasiri ya leo Juma Tano ya (30 Jamadil Aakhira 1438 h) sawa na (29 Machi 2017 m) imeanza wiki ya kitamaduni (Nasimu Karbala), inayo simamiwa na Atabatu Husseiniyya tukufu kwa kushirikiana na chuo cha Al-kauthar cha Pakistani, huku Ataba za Alawiyya, Askariyya na Abbasiyya zikishiriki.

Mtandao wa Alkafeel wa kimataifa umeandaa taarifa kuhusu ripoti ya siku ya kwanza ambayo ilikua kama ufuatavyo:

Kwanza: Saa kumi alasiri –kwa majira ya Pakistani- ilianza hafla ya ufunguzi, ilipata uwakilishi mkubwa kutoka katika Ataba za Iraq na jopo la wanadini, wanasiasa na wanatamaduni wa Pakistani, hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo somwa na msomaji wa Atabatu Alawiyya tukufu Sayyid Hussein Hakeem, kisha akaongea muwakilishi wa Marjaa dini mkuu katika nchi ya Pakistani na kiongozi mkuu (Mushrifu) wa chuo cha Al-kauthar muheshimiwa Shekh Muhsin Ali Najafi, ambaye aliwakaribisha wageni kutoka Iraq na akasema ni utukufu mkubwa sana kua pamoja na ndugu zetu kutoka Iraq, kwani wao wanabeba tamaduni za Ahlulbait (a.s) na mafunzo ya Karbala ambayo sie tuna haja nayo sana, yatupasa kumshukuru Mwenyezi Mungu mtukufu kwa hii neema kubwa, ndugu zangu wapakistani tunatakiwa tunufaike na ugeni huu mtukufu, watu wetu wanahitaji zaidi makongamano kama haya mbayo yanamafunzo makubwa.

Baada yake ulifuata ujumbe wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Husseiniyya tukufu ulio wasilishwa kwa niaba yake na muwakilishi wake Shekh Ali Qar-a’awiy.

Pili: hafla ya ufunguzi ikahamia katika uwanja wa chuo cha Al-kauthar, ambako zilifanyika shughuli ya kupandisha bendera za Ataba tukufu za Iraq (Alawiyya, Husseiniyya, Askariyya na Abbasiyya), ratiba hii ilipata mahudhurio makubwa sana kutoka kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wa Pakistani. Kuona zaidi fungua ukurasa wa Alkafeel wa kimataifa katika mtandao wa kijamii face book.

Tatu: Kufunguliwa kwa maonyesho ya bidhaa zinazo zalishwa na Ataba tukufu, ambayo yalihusisha matayi tofauti, pia kulikua na machapisho ya kielimu kwa lugha ya kiurdu na madirisha ya ziara kwa niaba, vitengo maalumu vya Ataba viliwekwa bendera za kubba tukufu ili watembeleaji wa vitengo hivyo wapate kutabaruku.

Fahamu kua kongamano na maonyesho haya yatadumu kwa siku tano Inshallah.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: