Katika siku ya kwanza ya Rajabu uliangaza mwanga wa kuzaliwa kwa imamu Muhammad Baaqir (aliyefanya haraka kupata elimu ya wamwanzo na wa mwisho)..

Maoni katika picha
Katika siku ya kwanza ya mwezi wa Rajabu Aswabu umma wa kiislamu hufanya kumbukumbu ya kuzaliwa nyota ya tano imamu Muhammad bun Ali Baaqir (a.s), aliye pata elimu ya wamwanzo na wa mwisho aliye zaliwa (57 h), akapokewa na Ahlulbait kwa shangwe ma furaha, kwani muda mrefu walikua wanasubiri kuzaliwa kwake kuliko bashiriwa na mtume wa Mwenyezi Mungu (s..a.w.w) kabla ya makumi ya miaka, akitokana na kizazi kitukufu, chenye watu bora wenye kila aina ya sifa ya ukamilifu wa ubinadamu, elimu, imani, akili, upole na tabia njema kwa ujumla.

Imamu Muhammad baaqir (a.s) ndiye imamu maasumu wa kwanza aliye tokana na wazazi wote wawili ambao ni Alawiyyaini, kwani yeye ni mtoto wa imamu Ali Zainul-abidina bun imamu Hussein bun imamu Ali bun Abuutwalib (a.s) hii ni nasaba ya ubabani kwake.

Tukiangalia upande wa mama yake, ni bibi mtukufu Fatuka binti imamu Hassan bun Ali bun Abuutwalib (a.s) na huitwa “Ummu Abdallah” alikua katika watukufu wa wanawake wa bani Hashim, imamu Zainul-abidina alikua anamwita Swidiqah, imamu Abuu Abdillahi Swaadiq (a.s) anasema: (Hakuwahi kupatikana katika kizazi cha Hassan mwanamke mfano wa Swidiqah) yatosha kua fahari kwake yeye ni pande la mjukuu wa mtume (s.a.w.w) na kwamba alilelewa katika nyumba alizo zitakasa Mwenyezi Mungu na zinazo litaja na kulitukuza jina lake tukufu, miguu ya mama huyu mtukufu ndio iliyo mlea imamu Baaqir (a.s).

Jina lake la kunia (baba fulani): Anaitwa Abuu Jafari (baba Jafari) hana kuniya nyingine zaidi ya hii.. amma kuhusu majina ya laqabu (sifa) anaitwa: (Ameen, Shabeeh –kwa sababu alikua anafanana sana na babu yake mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w)-, Shaakir, Haadi, Swaabir, Shaahid, Baaqir – hii ndio laqabu mashuhuri zaidi kwake- pia yeye na mwanaye imamu Swadi huitwa (Baaqiraini) kama wanavyo itwa pia (Swaadiqaini).

Imamu Baaqir (a.s) alipata elimu na maarifa kutoka kwa baba yake imamu Zainul-abidina (a.s), akawa na elimu ya hali ya juu kabisa kama alivyo tabiriwa na babu yake mtume (s.a.w.w) aliye mpa jina la sifa (laqabu) ya Baaqir, pale alipo sema: (Hakika yeye ataharakia elimu mapema) alipo wabashiria waislamu kuzaliwa kwake na nafasi kubwa atakayo kua nayo katika kuhuisha elimu ya sheria, katika zama ambazo umma wa kiislamu ulishuhudia ushindi wa mfululizo na mchanganyiko mkubwa wa watu na kuchanganyika kwa tamaduni.

Zama za imamu Baaqir (a.s) kulikua na mijadala na mazungumzo mengi ya kielimu, kwani ndio zama ambazo bani Umayya waliwapa nafasi wazushi na watu wenye misimamo mibaya, imamu Baaqir (a.s) akasimama imara kujibu hoja za wazushi hao na kuuelekeza umma katika njia iliyo nyooka.

Alijulikana (a.s) kwa ufasaha wa kuongea na uimara wa hoja katika nyanja ya Fiqhi, Mantik na Sheria, alikua anafanya vikao na wanazuoni wakubwa wanamuuliza maswali na kujadiliana, hakika walinufaika nae sana (a.s) imamu Muhammadi (a.s) wakati wote wa uhai wake katika mji wa Madina alikua anafundisha umma wa kiislamu, na kusimamia mambo ya kijamii yaliyo anzishwa na Mtume (s.a.w.w) na kuendelezwa na imamu Ali kisha imamu Hassan na Hussein (a.s) na kusitawishwa baada yao na baba yake Ali bun Hussein (a.s) watangulizi wake wana kila aina ya sifa nyema na ukamilifu, hii ni sababu kubwa ya utukufu wake.

Imamu Baaqir (a.s) aliishi na babu yake imamu Hussein (a.s) miaka mitatu na alishuhudia tukio la Karbala, na aliishi na baba yake imamu Sajjaad (a.s) miaka thelathini na nane akichota utukufu na elimu ya baba yake aliye kua na ubinadamu wa hali ya juu kabisa na aliongoza karibu miaka ushirini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: