Mwitikio mkubwa wa wadau wa maonyesho ya vitabu ya kimataifa huko Bagdad katika banda la Atabatu Abbasiyya tukufu..

Maoni katika picha
Kama kawaida yake katika kila maonyesho, banda la Atabatu Abbasiyya tukufu limepata muitikio mkubwa sana kutoka kwa wadau wa maonyesho ya vitabu ya kimataifa yanayo endelea hivi sasa katika mji mkuu wa Iraq Bagdad.

Kutokana na bidhaa zilizo shehena kwenye banda hilo chini ya kitengo cha habari na utamaduni na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, miongoni mwa vitabu na machapisho mbalimbali, wamepata nafasi kubwa katika ulimwengu wa elimu, limedhihirika hilo kutokana na mwitikio mkubwa wanaopata katika maonyesho ya vitabu na machapisho ya Ataba tukufu, katika nyanja ya elimu, tamaduni, turathi, na yote ni mazao halisi ya Ataba tukufu kuanzia uandishi hadi uchapaji, hii ndio sifa pekee ya Ataba ukilinganisha na vituo vingine..

Kwa mujibu wa watumishi wa banda hilo, vitu vinavyo pata muitikio mkubwa sana ni Mausuaat, Majarida ya kielimu na msahafu uliochapishwa na Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na machapisho ya turathi (habari kale), hali kadhalika vitabu vya uhakiki na muongozo wa watafiti wa vyuo vikuu unao chapishwa na maktaba ya Daru Makhtutwatu ya Atabatu Abbasiyya na vitabu vinavyo chapishwa na idara ya masomo mbalimbali.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imesha hudhuria mara nyingi maonyesho ya vitabu ya kimataifa ambayo hufanywa Bagdad, na huyachukulia kua maonyesho muhimu kwake, pamoja na maonyesho au makongamano mengine ambayo hufanywa ndani au nje ya Iraq yanayo endana na sera yake ambayo ni kueneza fikra na mafundisho ya Ahlulbait (a.s) vitengo vyake hupata muitikio mkubwa kutoka kwa watembeleaji (wadau) na hujitahidi kuongeza bidhaa mpya katika kila maonyesho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: