Nukta muhimu katika maisha ya imamu Ali Haadi (a.s)..

Maoni katika picha
Tupo katika siku za kukumbuka kuzaliwa kwa imamu wa kumi miongoni mwa maimamu maasumina (watakasifu) ambaye ni imamu Ali bun Muhamma Haadi (a.s).

Kuzaliwa kwake (a.s):

Alizaliwa katika kijiji cha Swarba karibu na mji wa Madina Munawwara, siku ya Juma Nne mwezi pili Rajabu Aswabu mwaka wa mia mbili kumi na mbili hijiriyya, yawezekana habari hii inaungwa mkono na alicho sema imamu Jawaad (a.s) katika dua ya mwanzo wa mwezi wa Rajabu, alipo sema: (Ewe Mwenyezi Mungu nakuomba kwa utukufu wa waliozaliwa katika mwezi wa Rajabu, Muhammad bun Ali na mwanaye Ali bun Muhammad mteule) bali inatilia mkazo habari hiyo, japo kua kuna riwaya zingine.

Jina na nasabu yake (a.s):

Anaitwa Imamu Ali bun Muhammad bun Ali bun Mussa bun Jafari bun Muhammad bun Ali bun Hussein bun Ali bun Abuutwalib (a.s).

Kunia yake (a.s):

Anaitwa Abul-hassan, pia huitwa Abul-hassan wa tatu; ili kumtofautisha na imamu Ali Ridhwa (a.s) kwani yeye ni Abul-hassan wa pili.

Laqabu zake (a.s):

Anaitwa, Haadi, Mutawakil, Fattaahu, Nnaqi, Murtadhwa, Najibu, A’alimu.. anatambulika zaidi kwa laqabu ya Haadi.

Mama yake (a.s) na mkewe:

Mama yake anaitwa bibi Sumana mtu wa Morocco, alikua mtumishi, na mke wake ni bibi Susan, pia alikua mtumishi.

Umri wake (a.s) na uimamu wake:

Aliishi miaka 42 na alikua imamu kwa miaka 33.

Watawala za zama zake (a.s):

Mu’utaswimu, Waathiqu, Mutawakkil.

Nakshi ya pete yake (a.s):

Ilikua imeandikwa; Kulinda ahadi ni miongoni mwa tabia za waja, na inasemekana ilikua imeandikwa maneno tofauti na hayo.

Miongoni mwa kauli za imamu Haadi (a.s):

  • 1- Alisema (a.s) [Atakaye ridhisha nafsi yake watakua wengi watakao mchukia].
  • 2- Alisema (a.s) [Msiba kwa mtu mwenye subira ni mmoja na asiye kua na subira hua misiba miwili].
  • 3- Alisema (a.s) [Mzaha ni pambo la punguani na kiwanda cha wajinga].
  • 4- Alisema (a.s) [Kukesha huleta ladha ya usingizi na njaa huongeza uzuri wa chakula].
  • 5- Alisema (a.s) [Kumbuka kifo chako mbele ya watu wako hakuna daktari wala rafiki atakaye kufaa].

Nafasi yake kielimu (a.s):

Wanahistoria wote wameandika kua; Imamu (a.s) alikua na elimu kubwa kushinda wanazuoni wote wa zama zake, Shekh Tusi ameandika katika kitabu chake (Rijaalu Tuusi) majina mia moja themanini na tano ya (wanazuoni) waliosoma kwake.

Miujiza yake (a.s):

Imamu Haadi (a.s) alikua na miujiza na karama zilizo andikwa na vitabu vya historia, miongoni mwake ni:

  • 1- Akiwa na umri wa miaka nane (a.s) alipokea rasmi madaraka ya uimamu, cheo hicho watu wazima hawakiwezi mbali na watoto ispokua kwa msaada wa Mwenyezi Mungu mtukufu.
  • 2- Mutawakkil aliamrisha aletewe simba watatu, akawaweka katika uwanja wa qasri lake, kisha akaingizwa imamu Haadi (a.s) sehemu hiyo na wakamfungia milango ili aliwe na simba, simba walimzuguka imamu (a.s) na wakawa wapole kwake, naye aliwashika shika manyoya ya shingoni, kisha alitoka na akamfuata Mutawakkil akiwa na zawadi, watu wakamuambia Mutawakkil: Mtoto wa Ammi yako (Imamu –a.s-) anacheza na simba na wewe fanya kama alivyo kua anafanya, Mutawakkil akawaambia: Mnataka kuniua! Kisha akawakataza wasiongelee habari hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: