Hivi ndio alivyopata shahada imamu Haadi (a.s)..

Maoni katika picha
Imamu Haadi (a.s) aliishi katika mji wa babu yake mtume -s.a.w.w- (Madina) karibu miaka ishirini, kisha Mutawakil Abbasiy akamtaka aende Samara, akaishi huko miaka ishirini hadi alipo uawa kwa sumu, na akazikwa katika nyumba yake mahala lilipo kaburi lake hadi sasa, baada ya kukaa jela kwa miaka mingi.

Imepokewa kutoka kwa Allaama Majlisiy (r.a) katika kitabu cha Jalaaul uyuun, kua imamu Ali Haadi (a.s) alipata shahada kwa sumu akiwa na miaka arubaini, pia inasemekana alikua na miaka arubaini na moja.

Alishika rasmi madaraka ya uimamu baada ya baba yake imamu Jawaad (a.s) akiwa na umri wa miaka sita na miezi mitano, na uimamu wake ulidumu kwa miaka thelathini na tatu na mwezi kadhaa.

Alipo ingia madarakani Mu’utamadi Abbasi –inasemekana Mu’utazi- alifuata siasa za Mutawakil, alimbana sana imamu Haadi, kutokana na nafasi kubwa aliyo kua nayo katika jamii, pamoja na kua hakua mfalme wala hakua na mali, alimuonea husuda na akapata dhiki katika nafsi yake kwa yale aliyo ona na kusikia kuhusu ukarimu na miujiza ya imamu Haadi (a.s) kama anavyo sema Mwenyezi Mungu: (Bali wanawafanyia husuda watu kwa yale waliyo pewa na Mwenyezi Mungu katika fadhila zake).

Uovu wake ukaanza kumsukuma kufanya jambo baya zaidi katika uislamu na kibinadamu, akamuwekea sumu imamu Haadi katika chakula chake, baada ya kula chakula chenye sumu imamu (a.s) akaugua hadi akapata shahada kutokana na sumu hiyo, kama walivyo kufa mashahidi baba zake na babu zake kabla yake.

Aliye muua imamu (a.s) ni Mu’utamad Abbasiy, kama alivyo sema ibun Baabawaihi na wengineo, na baadhi ya riwaya zingine zinasema aliye muua ni Mu’utazi Abbasiy.

Imamu Haadi (a.s) alifia katika mji wa Samara, mwezi tano Jamadil Aakhira, na inasemekana alifariki mwezi tatu Rajabu, pia inasemekana mwezi tatu Jamadil Aakhira mchana mwaka wa (254 Hijiriyya).

Imamu Askariy (a.s) aliswalia mwili mtukufu wa baba yake kisha akamzika katika nyumba yake, likasihi jina la siri kwa aliye ona (sirru man ra-aa) siku ya umauti wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: