Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s): Mwenyezi Mungu akupe malipo makubwa bwana wangu ewe Hussein kwa kufiwa na mjukuu wako Haadi..

Maoni katika picha
Mwenyezi Mungu akupe malipo makubwa bwana wangu ewe Hussein kwa kufiwa na mjukuu wako Haadi.. kwa maneno haya na mengine ya kuomboleza, watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) walimuambia imamu Hussein (a.s) katika kumbukumbu ya shahada ya mjukuu wake imamu Haadi (a.s) ambayo imeadhimishwa leo.

Maukibu (kundi) la pamoja la maombolezo lililo husisha watumishi wa malalo ya mwezi wa familia Abulfadhil Abbasi (a.s) na mazuwaru wake waombolezaji wa msiba huu mkubwa, waliimba qaswida na mashairi ya huzuni, na wakaenda katika malalo ya bwana wa mashahidi kumpa pole kutokana na msiba huu wenye majonzi makubwa, ulio wahuzunisha watu wa nyumba ya mtume mashukio ya wahayi, katika siku kama ya leo mwezi tatu Rajabu mwaka wa (254 Hijiriyya).

Walipo fika; walipokewa na watumishi wa Atabatu Husseiniyya tukufu wakaelea pamoja katika malalo yake matukufu huku wakiimba qaswida na mashairi ya maombolezo wakiwa wamejawa huzuni kubwa kufatia kifo cha imamu Haadi (a.s) mazuwaru wa imamu Hussein (a.s) kutoka ndani na nje ya Karbala walishiriki pia.

Kumbuka kua imamu Ali Haadi (a.s) alipata shahada kwa sumu akiwa na umri wa miaka arubaini, na inasemekana alikua na miaka arubaini na moja, aliyo pewa na Mu’utamad Abbasiy –na inasemekana alipewa na Mu’utazi- na alizikwa katika nyumba yake mahala lilipo kaburi lake hadi sasa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: