Watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wapata utukufu wa kuwatumikia mazuwaru wa maimamu wawili Askariyyain (a.s)..

Maoni katika picha
Kama kawaida yake katika misimu ya ziara zinazo fanyika katika malalo matukufu, Atabatu Abbasiyya imeshiriki katika ratiba iliyo pangwa na Atabatu Askariyya tukufu ya kupokea mazuwaru wa malalo ya maimamu wawili Askariyyain (a.s) katika kumbukumbu ya shahada ya imamu Haadi (a.s) ambayo leo mwezi tatu Rajabu Aswabu ndio kilele chake, wakinufaika na uzoefu mkubwa walio nao katika kuhudumia mamilioni ya mazuwaru katika Ataba za Karbala tukufu.

Kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu na katibu wake mkuu, limetumwa jopo la watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kwenda kushiriki na kusaidiana na Atabatu Askariyya tukufu katika kuhudumia mazuwaru wake watukufu, wametumwa huko kabla ya siku tano na wanafanya kazi bega kwa bega na ndugu zao watumishi wa Atabatu Askariyya tukufu.

Iliandaliwa ratiba maalumu na kugawa majukumu kwa kila mtu, shughuli zote zinafanywa kwa kufuata ratiba iliyo andaliwa na uongozi wa Atabatu Askariyya tukufu.

Watumishi walio enda kushiriki ni zaidi ya (150) na magari (28) yakiwemo magari (22) ya kubeba mazuwaru na mengine magari ya usafi na ya maji, na wamegawa zaidi ya blaketi (1,250).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: