Kamati ya maandalizi ya shindano la kitafiti yaongeza muda wa kupokea tafiti zitakazo shiriki katika shindano hilo..

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya shindano la kitafiti litakalo fanyika katika kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada la kumi na tatu yatangaza kuongeza muda wa kupokea tafiti zitakazo shiriki katika shindano hilo hadi tarehe 15 Rajabu badala ya tarehe 1 Rajabu, ili kutoa nafasi zaidi kwa washiriki, na wanatakiwa kutuma tafiti zao katika anuani zifuatazo:- rabee@alkafeel.net au almaaref@alkafeel.net au anahj.org@gmail.com .

Kamati imebainisha kua mabadiliko yamefanyika katika tarehe ya kupokea tafiti peke yake, mambo mengine yote yanabaki kama yalivyo pangwa, mada ni zile zile, ambazo ni:

Mada za Akhlaqi:

 • 1- Mwanadamu kamili mwenye maadili mema, imamu Hussein (a.s) kama mfano.
 • 2- Athari ya kutafakari katika kutambua nafsi na uokovu wake, Huru kama mfano.
 • 3- Uelewa wa kujitolea zaidi kibinadamu hadi unaathirika.. Abbasi (a.s) kama mfano.

Mada za fiqhi:

 • 1- Sababu za jihadi baina ya Twafu na Hashdi.. Fatwa ya Marjaa kama mfano.
 • 2- Ugaidi na misingi yake ya kifiqhi baina ya Twafu na makundi ya kitakfiri.
 • 3- Utukufu (heshima) ya damu, mali, cheo kwa wanaojisalimisha baina ya Ashuraa na leo.

Mada za kisheria na kisiasa:

 • 1- Haki za binadamu baina ya maneno ya Hussein (a.s) na mikataba ya kimataifa.
 • 2- Swala la haki na wajibu katika uelewa wa tukio la Twafu.
 • 3- Swala la mkazi na kiongozi katika ujumbe wa haki.
 • 4- Swala la mahakama huru katika kutengeneza jamii kufuatia uwanja wa ujumbe wa haki.

Mada za kibinadamu:

 • 1- Athari za hotuba za Husseiniyya katika kupambana na nidhamu za kifisadi.
 • 2- Misingi ya kuishi kwa amani katika mafunzo ya imamu Hussein (a.s).
 • 3- Ubinadamu katika maumbile ya imamu Hussein (a.s) kwa mwanachuoni mtafiti.
 • 4- Ukarimu wa mwanamke baina ya mafunzo ya Ashuraa na mafunzo mengine.. Hauraa Zainabu (a.s) kama mfano.
 • 5- Habari za kivita na mchango wake katika kuleta ushindi chini ya mtazamo wa vizito viwili.

Kuhusu masharti ya mashindano, kamati ya maandalizi imeweka kanuni na masharti ambayo lazima yazingatiwe katika shindano hili, kama ifuatavyo:

 • 1- Utafiti usiwe umesha wahi kutolewa au kuchapishwa na watu wengine kabla yako.
 • 2- Utafiti uandikwe kwa kufuata kanuni za kielimu.
 • 3- Usiandike chini ya kurasa (15) na zisizidi (30) uandike kwa hati ya (Arabic simplified) herufi saizi (14) na uhifadhi katika (CD).
 • 4- maneno yasizidi (300) uambatanishe na muhtasari wa utafiti wako.
 • 5- Utafiti wowote ambao hautazingatia mada tajwa hapo juu au hauta ambatanishwa na wasifu (CV) ya muandishi hautazingatiwa.
 • 6- Utafiti utumwe pamoja na wasifu (CV) ya muandishi, namba ya simu ya mkononi na email katika anuani ya barua pepe au zipelekwe moja kwa moja katika ofisi za kitengo cha maarifa ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu au katika ofisi za taasisi ya elimu ya Nahju Balagha ndani ya Atabatu Husseiniyya tukufu, tarehe ya mwisho ni (15 Rajabu 1438 h). kutakua na zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu.

Zawadi za washindi ni:

Mshindi wa kwanza (1,000,000) milioni moja dinari za Iraq.

Mshindi wa pili (750,000) laki saba na elfu hamsini dinari za Iraq.

Mshindi wa tatu (500,000) laki tano dinari za Iraq.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa barua pepe zifuatazo:- rabee@alkaleel.net au almaaref@alkafeel.net au inahj.org@gmail.com au piga simu namba zifuatazo: 0772843600 na 07723757532.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: