Tabia ya kuwasiliana na kutambuana na watu wa sekula pamoja na vyuo vikuu vya Iraq ambayo ni miongoni mwa ratiba za mradi wa kijana wa Alkafeel mzalendo unaofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kitengo cha mahusiano na vyuo, inahusisha mambo mengi, miongoni mwa mambo hayo ni kushirikiana na wahitimu katika mahafali yao sawa ifanyike katika vyuo vyao au katika Atabatu Abbasiyya, yote hayo hufanywa kwa kuwasiliana na viongozi wa vyuo husika, miongoni mwa vyuo hivyo ni chuo cha Teknolojia.
Imefanyika mahafali ya kuhitimu kwa wanafunzi katika moja ya kumbi zake na kuhudhuria ugeni rasmi kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu, mahafali ilikua tulivu inayo endana na hadhi ya mwanafunzi wa Iraq, ambaye ni nguzo muhimu ya jamii anaye tarajiwa kujenga nchi na kuleta maendeleo katika kila sekta.
Mahafali ilipata mahudhurio makubwa ya wahitimu pamoja na walimu wao wakiongozwa na rais wa chuo, yalifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ukaimbwa mwimbo wa taifa na ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu akaongea rais wa chuo dokta Ali Abdulhussein, aliwapongeza wahitimu na kuwatakia heri nyingi na baraka, aliwaambia kua: “Hakika maendeleo ya Nchi hii yanawategemea nyie kwa asilimia kubwa, nyie ndio wajenzi wa Nchi na ndio viongozi wake”. Pia aliwashukuru Atabatu Abbasiyya kwa ushiriki wao mzuri unao onyesha wazi namna wanavyo jali kundi hili muhimu katika jamii ya wairaqi.
Halafu ukafuata ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na Sayyid Muhammad Mussawiy kutoka katika kitengo cha dini, alianza kwa kuwapongeza wahitimu kwa kumaliza masomo yao na kuwataka waonyeshe ujuzi wao kwa kuijenga Iraq, akawasisitiza kua wafanye juhudi kubwa na wajitolee katika kujenga nchi na wajiepushe na kila kitakacho taka kupunguza ari yao katika kujenga nchi.
Kisha ukatolewa muhadhara elekezi na kiongozi wa idara ya utamaduni na habari za kimataifa kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Jasaam Said, aliwaambia wahitimu kuhusu umuhimu wa kujiendeleza na namna ya kuitumia elimu yao kwa kufuata maadili na maelekezo ya dini yoa tukufu.
Baada ya hapo wahitimu walisoma mashairi, mahafali ilihitimishwa kwa kumzawadia rais wa chuo ngao ya Atabatu Abbasiyya tukufu kutokana na juhudi kubwa anayo fanya, kisha vikagawiwa vyeti kwa wahitimu, walionyesha furaha kubwa kwa namna Atabatu Abbasiyya tukufu ilivyo wajali, na wakaomba ipanue ushiriki wake katika vyuo vingine pia.