Jioni ya Juma Pili (4 Rajabu 1438 h) sawa na (02 April 2017 m) ilimalizika ratiba ya wiki ya kitamaduni awamu ya nne (Nasimu Karbala) iliyo simamiwa na Atabatu Husseiniyya tukufu kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Alkauthar cha Pakistani, na kwa kushiriki Atabatu Alawiyya, Askariyya na Abbasiyya kuanzia tarehe (29 Machi hadi 02 April).
Hafla ya kuhitimisha ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, iliyo somwa na msomi wa Atabatu Askariyya tukufu Swaadiq Zaidiy, kisha akaongea muwakilishi wa Marjaa dini mkuu katika nchi ya Pakistani na kiongozi mkuu (mushrifu) wa chuo cha Alkauthar muheshimiwa Shekh Muhsin Ali Najafiy, alitoa shukrani kubwa kwa viongozi wa kisheria wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) muheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai na Sayyid Ahmad Swafi (d.i) pamoja na katibu mkuu wa Atabatu Alawiyya tukufu Sayyid Nizaar Hablulmatin na kiongozi wa Atabatu Askariyya tukufu Shekh Sataar Murshidiy, kwa kupeleka ugeni katika nchi hiyo iliyopo karibu sana na mwenendo wa Ahlulbait (a.s), akamuomba Mwenyezi Mungu kuidumisha neema hiyo kwa kuendelea kufanyika makongamano kama haya katika miaka ijayo inshallah.
Baada ya hapo ulifuata ujumbe wa Ataba tukufu ulio wasilishwa na Shekh Aadil Wakil.
Kisha wakavishwa mataji wanafunzi walio hitimu masomo katika chuo cha Alkauthar na wakavishwa vilemba, halafu ikapigwa kura ya kuchagua watu (20) watakao faulu kwenda kutembelea Ataba za Iraq, watu (10) watagharamiwa na Atabatu Husseiniyya na (10) wengine watagharamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu.
Pia hafla ilishuhudi autolewaji wa zawadi wa pande mbili baina ya chuo cha Alkauthar na wageni waliokuja kushiriki katika ratiba ra wiki hii kutoka katika Ataba tukufu za Iraq.