Kuthamini mihanga ya baba zao: Atabatu Abbasiyya tukufu yawazawadia watoto wa mashahidi wanaosoma katika shule za Abulfadhil Abbasi (a.s)..

Maoni katika picha
Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi, alafu akaongea kiongozi wa Scaut dokta Zamaan Kinaniy, alielezea utukufu wa shahidi na nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu na akapongeza namna mashahidi walivyo jitoa muhanga.

Akabainisha kua: “Hakika kuwakumbuka mashahidi na familia zao ni deni kwetu, jambo dogo sana tunalo weza kuwafanyia ni kuzikirimu familia zao kutokana na utukufu wa damu walizo mwaga kwa ajili ya kutufanya tuishi kwa amani na kuilinda nchi yetu na maeneo matukufu, leo tumekaa hapa kuenzi utukufu wa shahidi na kuendelea kusimamia malengo yao yaliyo sababisha wapate shahada, waliitikia wito wa Marjaa dini mkuu wakanusuru haki na kuangamiza batili hakika wanastahiki kuenziwa kwa kiwango cha juu kabisa”.

Kiongozi wa idara ya harakati na mahema, Ustadhi Ali Hussein Abduzaid aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Miongoni mwa harakati za idara ya Scaut ya Alkafeel chini ya Jumuiya ya Scaut ya Alkafeel ya kusaidia mayatima wa wapiganaji wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi, harakati hii imefanya mambo mbalimbali yanayo lenga kusaidia watoto wa mashahidi na familia zao, ratiba yetu ya leo ni kutoa zawadi kwa watoto wa mashahidi wanao soma katika shule za Abulfadhil Abbasi (a.s) zilizo chini ya Ataba tukufu, tumetoa zawadi kwa watoto zaidi ya ishirini, pamoja na kuwaingiza watoto hao katika harakati zinazo fanywa na mahema ya Scaut, hii ni sehemu ya kuonyesha thamani ya namna baba zao walivyo jitolea damu na nafsi zao kwa ajili ya kulinda nchi yetu na raia wake pamoja na maeneo matukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: