Kamati imetangaza kanuni na masharti ya kushiriki katika shindano hili kama ifuatavyo:
- 1- Picha ionyeshe ushujaa wa jeshi na Hashdi Sha’abi pamoja na misimamo yao ya kiubinadamu kuhusu wakimbizi na maeneo yenye matatizo.
- 2- Mshiriki anaruhusiwa kua na picha tano hadi kumi na zisiwe na maandishi yeyote au jina.
- 3- Baada ya picha kuingizwa katika shindano hairuhusiwi kufanyiwa marekebisho yeyote.
- 4- Picha zisiwe na ujumbe wowote wa kikundi au watu fulani, bali zinaruhusiwa kua na alama za bendera za Hashdi Sha’abi au bendera ya taifa la Iraq.
- 5- Ziwe na ukubwa wa kati ya saizi (2000) hadi (3000).
- 6- Picha zionyeshe ushiriki wa wapiganaji katika matukio.
- 7- Picha zihifadhiwe katika albam maalumu itakayo wasilishwa katika shindano au zihifadhiwe katika (CD) na ziwasilishwe kwenye kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na jina la mchoraji au zitumwe kwa barua pepe kwenye anuani hii: (info@holyfatwa.com).
- 8- Picha yeyote ambayo haitakidhi vigezo tajwa hapo juu haitazingatiwa.
- 9- Picha zitakazo shiriki katika shidano zitabaki chini ya umiliki wa Atabatu Abbasiyya tukufu na wao ndio wenye haki ya kuzisambaza.
- 10- Mwisho wa kupokea picha ni (05/05/2017 m).
- 11- Washidi watatu wa mwanzo watapewa zawadi kama ifuatavyo:-
Mshindi wa kwanza 750,000 dinari za Iraq pamoja na kidani.
Mshindi wa pili 500,000 dinari za Iraq pamoja na kidani.
Mshindi wa tatu 250,000 dinari za Iraq pamoja na kidani.