Aina 108 za ubunifu zitashiriki katika maonyesho ya kwanza ya wabunifu yatakayo anza kesho Juma Tano..

Maoni katika picha
Muhandisi Manar Atwa-llah Ali Sa’adiy mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano na maonyesho ya kwanza ya wabunifu yatakayo anza kesho Juma Tano ya tarehe 05/04/2017 m, chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na chama cha wabunifu wa kiiraq, ametangaza kua idadi ya aina za ubunifu zitakazo shiriki katika maonyesho hayo imefika 108, baada ya kufanya mchujo wa aina 500 zilizo wasilishwa, ubunifu huo unalenga mambo matano ambayo ni: (Utabibu, Uhandisi, Elimu, Kilimo na Jeshi).

Akaongeza kusema kua: “Vimezingatiwa vigezo vinavyo kubalika katika kuteua aina za ubunifu utakao shiriki katika shindano chini ya wataalamu wa Atabatu Abbasiyya tukufu na wametumia vipimo vya kimataifa vinavyo tumika katika maonyesho ya ubunifu ya kimataifa, miongoni mwa vigezo muhimu ni:

  • 1- Ubunifu uwe umepata shahada ya ubunifu kutoka katika kituo cha ubunifu kinacho kubalika itakayo onyesha kiwango na aina ya ubunifu.
  • 2- Uwe ndani ya muda wa dhamana ambao ni chini ya miaka 20, kwa sababu ubunifu hua unakinga ya dhamana ya miaka ishirini.
  • 3- Ubunifu uwe ambao ukitekelezwa utaleta faida kubwa kwa taifa hasa katika mazingira ya sasa.
  • 4- Ubunifu uwe unaweza kuleta manufaa hivi sasa na kwa gharama ndogo.
  • 5- Malighafi za ubunifu huo ziwe zinapatikana hapa Iraq kuepusha gharama ya kuagiza malighafi nje ya nchi.

Akabainisha kua: “Kazi ya kuchuja ubunifu ilifanyika bila kua na majina ya wabunifu husika, kazi zao zilipewa namba na baada ya kupasishwa ndio yakaandikwa majina ya wahusika wa ubunifu huo, na kila mbunifu anatakuwa kua na aina moja tu ya kazi ya ubunifu wake”.

Kamati imetangaza kukamilika kwa maandalizi yote ya kongamano na maonyesho yatakayo anza kesho saa nane mchana chini ya kauli mbiu: (Karbala ni chemchem ya elimu na wanazuoni) litakalo fanyika katika ukumbi wa jengo la Kuleiniy lililo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika barabara ya Bagdad – Karbala la litaendelea hadi tarehe: 07/04/2017m.

Hafla ya ufunguzi itakua na maneno ya ukaribisho na utambulisho wa kongamano pamoja na ujumbe wa shirika la kudhibiti viwango la Iraq halafu yatafunguliwa rasmi maonyeshi ya ubunifu.

Kumbuka kua kongamano na maonyesho haya yanalenga kusaidia wabunifu na kuwezesha kunufaika na ubunifu wao pamoja na kushajihisha wananchi wa Iraq kuboresha ubunifu wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: