Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya mahusiano na vyuo kwa kushirikiana na uongozi wa malezi wa mkoa wa Misaan wamehitimisha shindano la kijana wa Alkafeel lililo husisha wanafunzi wa shule za upili (sekondari) yanayo lenga kulea wanafunzi kimaadili, elimu na kidini.
Hafla ilifanyika katika ukumbi wa jengo la uongozi wa malezi wa mkoa wa Misaan, ilipata mahudhurio makubwa ya walimu na wanafunzi, ilianza kwa ufunguzi wa Qur’an tukufu halafu ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha ukaimbwa mwimbo ya taifa na mwimbo ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Baada ya hapo; Shekh Ali Asadiy kutoka katika kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu akapanda mimbari na kutoa hotuba, miongoni mwa aliyo sema ni: “Lazima tufahamu kua sheria ya kiislamu imetilia umuhimu sana elimu na imeipa heshima kubwa, Mwenyezi Mungu mtukufu amebainisha jambo hili mara nyingi ndani ya Qur’an, pia kuna hadithi nyingi kutoka kwa mtume (s.a.w.w) akihimiza kutafuta elimu na kuelezea utukufu wake, elimu ina nafasi kubwa sana katika jamii na umma kwa ujumla, miji inajengwa kutokana na elimu na umma unaheshimika kwa sababu ya elimu”.
Akaongeza kusema kua: “Mwalimu ana nafasi kubwa sana katika kutengeneza jamii bora, atakapo kua anafundisha na kuonyesha tabia nzuri na ikhlasi, mwanafunzi atapata elimu pamoja na maadili mema, mwalimu ni msingi muhimu katika kujenga wanafunzi, ukiwepo ushirikiano mzuri baina ya mwalimu na mwanafunzi mafanikio hupatikana, tuna haja kubwa ya kuifanya elimu kua ndio mnara wetu, kutokana na dhana hii Atabatu Abbasiyya tukufu ilianzisha mradi utakao saidia kujenga ushirikiano wa karibu na walimu kwa namna mbalimbali na miongoni mwake ni haya mashindano”.
Halafu ukafuata ujumbe wa kituo cha malezi cha mkoa wa Misaan ulio wasilishwa na mkuu wa idara Sayyid Baasim Nuuriy, alisema kua: “Pongezi kwetu kwa kufanyika mashindano ya kijana wa Alkafeel katika mkoa wetu mwaka huu, sisi tunashukuru sana na kupongeza kazi zinazofanywa na Ataba tukufu kuanzia katika viwanja vya utukufu na ushujaa ambako wanapigana vita vikali dhidi ya viumbe waovu zaidi duniani wajukuu wa Yazidi Madaesh, hadi katika kazi ya mitume ya kulea wanafunzi kwa mapenzi makubwa na imani ya hali ya juu na kuwafania wema, tunatarajia kuendelea kwa harakati hizi kutokana na faida kubwa inayo patikana kwa wanafunzi wetu pamoja na walimu watukufu, na linalo tufurahisha zaidi ni kua chini ya hema la yule tunaye jisalimisha kwake na kumsadikisha halifa wa mtume na mjukuu mtukufu muongoaji wa walimwengu na wasii aliye fikisha ujumbe”.
Baada ya hapo likasomwa shairi lenye anuani ya: (Sisi ni wapenzi wa Mwenyezi Mungu). Kisha Atabatu Abbasiyya ikagawa zawadi kwa viongozi wa kitengo cha malezi cha Misaan na kitengo cha harakati za shule na mwisho wakapewa zawadi wanafunzi walio faulu katika mashindano ambayo walishiriki jumla ya wanafunzi (2,100) na walio shinda ni (67) wanafunzi wa kiume na wakike, chini ya kanuni na masharti yaliyo wekwa katika mashindano.