Rais wa jukwaa la wabunifu wa kiiraq: Kupitia kongamano na maonyesho ya kwanza ya ubunifu tunaangazia akili bunifu za wairaq..

Ustadh Zaiduna Khalfu Saidiy
Rais wa jukwaa la wabunifu wa kiiraq Ustadh Zaiduna Khalfu Saidiy amebainisha kua, kongamano na maonyesho ya kwanza ya wabunifu yanayo fanyika chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu yanalenga kuamsha akili za wabunifu wa kiiraq na kuweka kanuni zitakazo saidia kubadilisha fikra kua vitendo halisi vyenye mashiko na manufaa.

Aliyasema hayo katika hotuba aliyo toa wakati wa ufunguzi wa kongamano na maonyesho ya kwanza ya wabunifu yaliyo anza adhuhuri ya Juma Tano (7 Rajabu 1438 h) sawa na (05/04/2017 m) na yatadumu siku tatu chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kusaidiana na jukwaa la wabunifu wa kiiraq chini ya kauli mbiu: (Karbala ni chemchem ya elimu na wanachuoni).

Akaongeza kusema kua: “Hakika ni furaha kubwa sana kufanyika kwa kongamano na maonyesho ya kwanza ya wabunifu chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ukarimu mkubwa ambao haupatikani ispokua kwa watu waliorithi utukufu wa Ahlulbait (a.s), maonyesho haya yanaenda sambamba na ushindi wa jeshi na Hashdi Sha’abi katika vita ya kukomboa mji wa Mosul”.

Akabainisha kua: “Jukwaa la wabunifu wa kiiraq lililo anzishwa ili liwe kimbilio la wabunifu waliopo ndani na nje ya Iraq kwa mara ya kwanza katika historia ya Iraq, kwa kutegemea kanuni ya 30 ya mwaka 1931, iliyo pelekea jopo la ngugu zenu wabunifu na walimu wa vyuo kuanzisha jukwaa la wabunifu linalo fiti katika misingi ya kielimu, ili likusanye zaidi ya wabunifu (300) wa kiiraq wanao fanya kazi kwa kujitolea bila kupata msaada sehemu yeyote ile”.

Akaendelea kusema kua: “Baada ya mafanikio tuliyo pata katika maonyesho yaliyo pita, ambapo mara ya mwisho yalikua maonyesho ya nguvu za umeme chini ya wizara ya mafuta katikati ya mwezi wa kumi na mbili ulio pita, na maonyesho ya teknolojia na ufundi, pamoja na kushiriki katika maonyesho na makongamano ya kimataifa, mara ya mwisho tulishiriki katika maonyesho ya kimataifa yaliyo fanyika nchini Misri ambako tulipata nafasi ya kwanza katika jumla ya nchi (15) washiriki”.

Akabainisha kua: “Katika maonyesho haya kuna aina za ubunifu (108) kutoka katika jumla ya aina (570) zilizo wasilishwa na kufanyiwa mchujo hadi kubakia hizo, ambazo zinalenga mambo matano (Utabibu, Uhandisi, Elimu, Kilimo na Jeshi)”.

Akamaliza kwa kusema kua: “Tunajitahidi kupitia maonyesho na kongamano hili kuangazia na kuamsha akili za wabunifu wa kiiraq na kuweka kanuni na taratibu zitakazo saidia kubadilisha fikra na kua vitendo halisi vyenye mashiko na manufaa, kutokana na kushiriki kwa mashirika yakitaifa na vikundi vya maendeleo vinavyo weza kuchangia mafanikio na ufanisi wa wabunifu ili kuleta maendeleo ya kiuchumi na kielimu, na kufanikisha kupatikana kwa maendeleo ya wabunifu tunayo yatafuta”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: