Baada ya serikali kushindwa kuwafadhili na kuwasaidia: Atabatu Abbasiyya tukufu yafadhili kongamano na maonyesho ya kwanza ya wabunifu wa kiiraq..

Sehemu ya halfa ya ufunguzi
Katika juhudi ya kusaidia vipawa vya akili za wairaq na kuhakikisha vinaleta manufaa kwa nchi, baada ya adhuhuri siku ya Juma Tano (7 Rajabu 1438 h) sawa na (05/05/2017 m) chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kwa kushirikiana na jukwaa la wabunifu wa kiiraq lilifunguliwa kongamano na maonyesho ya kwanza chini ya kauli mbiu isemayo (Karbala ni kituo cha elimu na wanazuoni) na litaendelea siku tatu katika jengo la Shekh Kuleiniy lililo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ushiriki mkubwa wa wanazuoni wa kidini na kisekula pamoja na watafiti wa Iraq, wakiwemo na wawakilishi wa Ataba na Mazaru tukufu, na jopo la viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wakiongozwa na kiongozi wao mkuu wa kisheria Sayyid Ahmad Swafi (d.i) na katibu wake mkuu Muhandisi Sayyid Muhammad Ashiqar (d.t).

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fatha maalumu kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq na wanazuoni walio tangulia, halafu ukaimbwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya.

Ukafuatia ujumbe wa kamati iliyo fadhili kongamano na maonyesho haya –Atabatu Abbasiyya- uliotolewa na kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmad Swafi (d.i) alibainisha kua: “Tutaendelea kulinda raia wa Iraq na taifa letu pamoja na maadili yetu na uwezo wetu, tutaendelea kupampana hadi mwisho, hatutaki kitu chochote bali tunataka mambo yakae sawa”.

Baada yake ukafuata ujumbe wa jukwaa la wabunifu uliowasilishwa na rais wa jukwaa hilo Ustadh Zaiduna Khalfu Saidiy ambaye alisema kua: “Hakika kongamano na maonyesho ya kwanza ya wabunifu yanayo simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu tunajitahidi kuangazia na kuamsha akili pevu za wabunifu wa kiiraq na kuweka kanuni zitakazo saidia kubadilisha fikra kua vitendo halisi vyenye mashiko na manufaa”.

Kisha akaongea rais wa kituo cha ubora na udhibiti wa viwango cha Iraq, Ustadh Saadi Abdulwahaab, alionyesha umuhimu mkubwa kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kusimamia kongamano na maonyesho ya wabunifu kwa mara ya kwanza ambao ni mwanzo mzuri wa kusaidia kundi hili muhimu la wanazuoni wabunifu wa kiiraq.

Baada ya hapo wahudhuriaji walikaribishwa kwenda kufungua maonyesho ya ubunifu na Muhandisi Manaar Atwallah Sa’adiy mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano na maonyesho ya kwanza ya wabunifu na alibainisha kua; Aina za ubunifu unao shiriki katika maonyesho haya ni (108) ambao umechujwa kutoka katika aina (570) zilizo wasilishwa, na ubunifu huo unahusu mambo matano ambayo ni: (Utabibu, Uhandisi, Elimu, Kilimo na Jeshi) akaongeza kusema kua: “Tulizingatia vigezo vinavyo kubalika kiubunifu katika kuchagua aina zitakazo shiriki maonyesho haya kupitia jopo la wataalamu wa Atabatu Abbasiyya na kutoka katika jukwaa la wabunifu na tulitumia vipimo vya kimataifa vinavyo tumika katika maonyesho ya aina hii duniani, na mambo muhimu ni:
    • 1- Ubunifu uwe umepata shahada ya ubunifu kutoka katika kituo cha ubunifu kinacho kubalika itakayo onyesha kiwango na aina ya ubunifu.
    • 2- Uwe ndani ya muda wa dhamana ambao ni chini ya miaka 20, kwa sababu ubunifu hua unakinga ya dhamana ya miaka ishirini.
    • 3- Ubunifu uwe ambao ukitekelezwa utaleta faida kubwa kwa taifa hasa katika mazingira ya sasa.
    • 4- Ubunifu uwe unaweza kuleta manufaa hivi sasa na kwa gharama ndogo.
    • 5- Malighafi za ubunifu huo ziwe zinapatikana hapa Iraq kuepusha gharama ya kuagiza malighafi nje ya nchi.

Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: