Kamati ya usuluhishi ya rais wa Urusi yatembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na kukagua miradi yake..

Maoni katika picha
Miongoni mwa ziara zinazo fanywa na kamati ya usuluhishi ya rais wa Urusi Putin, kamati hiyo imezuru Atabatu Abbasiyya tukufu, ikiwa ni sehemu ya ziara yao katika mkoa wa Karbala kwa ajili ya kuweka makubaliano na serikali ya mkoa, pamoja na kuunga undugu (urafiki) baina ya Karbala na moja ya mikoa ya kiviwanda ya Urusi.

Ugeni huo uliongozwa na rais wakamati hiyo bwana Andereya Ikoroof na waliongozana na ugeni wa China chini ya rais wa kamati ya uchumi wa China na Urusi bwana Kolodan Nei, walipokelewa na mudiru (mkuu) wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Haji Jawaad Hasanawiy, baada ya kuwakaribisha wageni, aliwapa maelezo kuhusu miradi tofauti ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ya ujenzi, uchumi, elimu na mingineyo, kisha ugeni ulitembea katika korido za Atabatu Abbasiyya na kuangalia ufanisi wa mradi wa upanuzi wa Ataba na upauaji wa paa la haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na mradi wa mawasitiano na ulinzi, baada ya kumaliza jaula (matembezi), bwana Andereya Ikoroof alisema kua: “Hakika lengo la kwanza la ziara yetu ni kujenga uhusiano bora na Iraq, na hatua ya kwanza ilikua ni kutembelea sehemu takatifu katika mji wa Karbala tukufu, kisha tukutane na serikali ya ndani ya mkoa wa Karbala, tumekuja kutoka Urusi kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za usuluhishi zinazo fanywa na rais Putin, na tumekuja kutembelea mji mtukufu wa Karbala kutokana na umuhimu wake kihistoria katika nchi ya Iraq, mapendekezo yetu ni kuunga undugu (urafiki) baina ya mkoa wa Karbala na moja ya mikoa ya kiviwanda ya Urusi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: