Ilipo tangazwa kupokea vifaa vya ubunifu vitakavyo shiriki katika maonyesho ya ubunifu ya kwanza yaliyo anza jana Juma Tano kwa kusimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu ikishirikiana na jukwaa la wabunifu wa kiiraq, pamoja na ufupi wa muda ulio tolewa pia umbali wa sehemu ya maonyesho ukitokea katika Ataba tukufu lakini maombi ya ushiriki yalifika (570), kwa kutumia vigezo vya ubunifu na kanuni za kimataifa, yakachujwa hadi kubakia (108) ndio yakapasishwa kushiriki katika maonyesho haya, vilizingatiwa vitu muhimu vinavyo weza kutekelezwa kwa gharana nafuu na kuleta manufaa makubwa katika sekta tano ambazo ni: (Utabibu, Uhandisi, Elimu, Kilimo na Jeshi).
Ujumbe wa maonyesho haya ambayo tunatarajia kuona maonyesho mengine ya aina hii siku za mbele, ukadhihirisha kua; Hakika wairaq wamekomaa kiakili na wana uwezo mkubwa wa ubunifu pamoja na mazingira magumu wanayo pitia.
Anaye tembelea korido za maonyesho atashangaa na kujiuliza namna gani akili iliweza kufikiri na kubuni vitu kama hivi, utaona ni wajibu kwa kila mtu sawa awe kiongozi wa serikali au raia wa kawaida kusaidia fikra hizi, na kuziingiza katika utendaji halisi, kwa ajili ya kuleta huduma mpya na bora inayo endana na maendeleo ya dunia ya sasa.
Ukizingatia kua vitu vinavyo onyeshwa vinahitajiwa na nchi yetu katika mazingira ya sasa, kama vile zana za kijeshi, kitabibu na kilimo, vitu hivyo vinagusa moja kwa moja maisha ya wairaq, kwa ufupi vitu vyote vilivyopo katika maonyesho haya vinaweza kutatua matatizo mengi ya wairaq iwapo vitaingizwa katika utendaji halisi.
Mtandao wa Alkafeel ulitembelea korido za maonyesho hayo na ukapiga picha baadhi ya vitu vilivyopo katika maonyesho