Alasiri siku ya Ijumaa (9 Rajabu 1438 h) sawa na (07/04/2017 m) lilihitimishwa kongamano na maonyesho ya kwanza ya wabunifu yaliyo fanyika chini ya kauli mbiu isemayo: (Karbala ni kituo cha elimu na wanazuoni) kwa usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu ikishirikiana na jukwaa la wabunifu wa kiiraq lililo dumu siku tatu.
Hafla ya kufunga maonyesho hayo ilifanyika katika uwanja wa jengo la shekh Kuleiniy lililo chini ya Ataba tukufu na kuhudhuriwa na watu muhimu wengi wa kidini na kisekula, wakiwemo viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wakiongozwa na kiongozi wao mkuu wa kisheria Sayyid Ahmad Swafi (d.i) na katibu mkuu Muhandisi Sayyid Muhammad Ashiqar (d.t). Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukaimbwa wimbo wa taifa na wimbo wa Ataba tukufu, kisha katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Muhandisi Muhammad Ashiqar akaongea, miongani mwa aliyo sema ni: “Hakika nchi yetu ya Iraq inauwezo mkubwa wa elimu za kisekula na elimu za kazi na historia, tunaweza kutumia ujuzi wetu katika kukuza uchumi na kujenga nchi”.
Pia kulikua na ujumbe kutoka katika kamati ya maandalizi ya kongamano na maonyesho haya, ulio wasilishwa na dokta Ali Adham mjumbe wa kamati hiyo, alisema kua: “Tutajitahidi kupitia Atabatu Abbasiyya tukufu kuangalia namna ubunifu huu unavyo weza kuchangia katika kujenga nchi yetu, na kubadilisha mawazo kua vitendo halisi, na kuwashajihisha wazalishaji kutumia fikra hizi zinazo weza kutekelezwa”.
Baada ya hapo; akapewa zawadi dokta Ali Bahadeli waziri wa kilimo wa zamani na mmoja wa wanachuoni maarufu na mtu mwenye uvumbuzi mwingi katika sekta ya kilimo, na amesha pata shahada za kitaifa na kimataifa na ana filamu inayo onyesha mafanikio yake na uzoefu alio nao katika sekta ya kilimo, hasa kilimo cha tende.
Likafuata tangazo la washindi katika kila aina ya ubunifu miongoni mwa zile aina tano (Utabibu, Uhandisi, Elimu, Kilimo na Jeshi) na zikagawiwa midani za Dhahabu, Fedha na Bronze.
Kisha ikatolewa zawadi kwa washiriki wote wa ubunifu (108) pamoja na kuwapa zawadi wajumbe wa kamati zilizo simamia na kuchangia mafanikio ya kongamano na maonyesho haya.