Tarehe 10 Rajabu kuzaliwa kwa nuru ya tisa katika nyumba ya Mtume (s.a.w.w) imamu Muhammad Jawaad (a.s)..

Maoni katika picha
Umma wa kiislamu unapitia siku ya kumi katika mwezi wa Rajabu Aswabu, ambayo ni siku ya kumbu kumbu ya kuzaliwa nuru ya tisa ambaye ni imamu Muhammad Jawaad (a.s) aliye julikana kwa kiwango cha juu cha elimu yake na juhudi kubwa aliyo fanya ya kufundisha madrasa ya Ahlulbait (a.s) na kuhakikisha inakua endelevu kwa kuwafundisha wanachuoni na wanafunzi njia za kujifundisha elimu ya sheria ya kiislamu yenye utajiri mkubwa.

Imamu Jawadi, ni Muhammad bun Ali bun Mussa bun Jafari bun Muhammad bun Ali bun Hussein bun Ali bun Abuutwalib (a.s), mama yake anaitwa bibi Sukaina Marsiyya, na inasemekana anaitwa Khaizaraan, na mke wake alikua anaitwa bibi Samana Mmorocco, imamu alikua anawaheshimu na kuwatukuza sana wafuasi wa Ahlulbait (a.s).

Imamu Muhammad Jawaad (a.s) alilelewa katika nyumba ya utume na uimamu, nyumba ambayo Mwenyezi Mungu amewatukuza waislamu kutokana na utukufu wa nyumba hiyo, alipata malezi bora kutoka kwa baba yake imamu Ridha (a.s), alikua anafuatana nae anapokua nyumbani au safarini hadi alipo kua mkubwa (a.s), alisoma kwa baba yake hadi akawa na kiwango cha juu kabisa cha elimu na aliwafundisha watu namna ya kusoma sheria ya kiislamu na akawahimiza kuandika na kuhifadhi wanayo someshwa na waliyo pokea kutoka kwa maimamu watakasifu.

Miongoni mwa majina yake ya laqabu (sifa) anaitwa: (Jawaad, Taqiyyu, Zakiyyu, Qaanii, Murtadha, Muntajab) anajulikana zaidi kwa laqabu ya (Jawaad) kutokana na ukarimu wake, pia aliitwa (Babu Muraad) baada ya kufariki kwake kutokana na watu kukidhiwa haja zao wanapo kwenda kumuomba Mwenyezi Mungu katika kaburi lake tukufu, aliishi miaka (25) na alikua imamu kwa miaka (17).

Kuhusu kuzaliwa kwake, bibi Hakima binti Abuu Hassan Mussa bun Jafar (a.s) anasimulia karama alizo ziona akisema: Ulipo fika muda wa kujifungua mama Abuu Jafari (a.s) alinita imamu Ridha (a.s) akasema: (Ewe Hakima kaangalie kuzaliwa kwake) nikaingia pamoja naye ndani ya nyumba, akatuwekea taa, kisha akatufungia mlango, tulipo sikia mlango unagongwa taa likazimika, nikashikwa na butwaa kwa kuzimika taa, tukaona kama mwezi wa Abuu Jafari katika chombo na kuna kitu laini kama nguo, kinatoa nuru kubwa ikaangaza chumba chote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: