Kituo cha kurepea nakala kale cha Atabatu Abbasiyya tukufu chashiriki katika kongamano la kielimu kuhusu athari katika chuo cha Kufa..

Maoni katika picha
Miongoni mwa mfululizo wa mawasiliano na vyuo pamoja na taasisi za kisekula Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kituo cha kurepea na kutunza nakala kale chini ya ofisi ya Daru Makhtutwaat katika Atabatu Abbasiyya imeshiriki katika kongamano la kielimu la kwanza kuhusu athari, linalo fanyika katika kitivo cha athari cha chuo kikuu cha Kufa chini ya kauli mbiu isemayo: (Athari zetu ndio msingi wa fahari yetu), katika ushiriki huo tulipata nafasi ya kutoa hotuba ya kitafiti iliyo tolewa na mmoja wa watumishi wa kituo hiki iliyo kua na anuani isemayo: (Madhara yanayo zipata nakala kale.. athari zake na utunzaji wake), kongamano hili linalenga kuangalia changamoto zinazo zikumba athari na turathi za Iraq, zaidi athari za mji wa Nainawa zilizo haribiwa na genge la magaidi na matakfiri ya daesh.

Mtaalamu mshiriki Ustadh Ali Abdulhussein aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kongamano hili limebeba mada nyingi, miongoni mwake ni urepeaji wa nakala kale na utunzaji wake, kwakua katika kituo cha kurepea nakala kale tuna uzoefu mkubwa wa swala hili tuliwasilisha mada ya kitafiti kuhusu madhara yanayo zipata nakala kale, kwa kutoa mfano halisi wa nakala kale moja tuliyo irepea katika kituo chetu ambayo ni (Muujazu fil-twib)”.

Akaongeza kua: “Tulipitia hatua muhimu kadhaa katika kurepea, kuanzia kuipokea na kuchunguza madhara iliyo nayo kisha kuitengenezea alama yake maalumu ya utambulisho, halafu tukaangalia namna ya kuiingiza katika vipimo vya kibaiolojia kwa ajili ya vipimo zaidi na kubaini sehemu zilizo haribika, baada ya hapo ikaingizwa kwa mkemia kwa ajili ya kupima wino uliotumika, kisha ndio inaingizwa katika hatua ya kurepea, ambayo huwa na njia mbili: njia ya kwanza ni kavu nayo ni kutumia karatasi za Japani, njia ya pili ni mbichi nayo ni kutumia uji wa karatasi kwa kufuata wasifu wa karatasi”.

Akabainisha kua: “Baada ya kumaliza kazi ya kurepea nakala kale hushonewa mfuko na kutengeneza jarada la nje, na hatua ya saba ni kutengeneza mfuko maalumu wa kuhifadhia kitabu, hapo kazi inakua imekamilika kuanzia kupokea hadi kuihifadhi katika mfuko wake tena kwa kufuata kiwango cha joto na baridi maalumu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: