Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya hafla ya kufikisha miaka ya kuwajibikiwa na sheria kwa wanafunzi wa shule ya msingi Abuutwalib ya wavulana na yazindua mashindano ya kielimu..

Maoni katika picha
Chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha malezi na elimu ya juu, shule ya msingi Abuutwalib ya wavulana ambayo ni miongoni mwa shule za Abulfadhil Abbasi (a.s) siku ya jana Juma Mosi (10 Rajabu 1438 h) sawa na (8 April 2017 m) wamefanya hafla ya kufikisha kwa miaka ya kuwajibikiwa na sheria kwa wanafunzi wake, pamoja na kuzindua aina mbalimbali za mashindano ya kielimu, hafla hii ni miongoni mwa sherehe za kuzaliwa kwa maimamu watakasifu (a.s) katika mwezi huu mtukufu wa Rajabu.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukaimbwa wimbo wa taifa, wanafunzi wakasoma utenzi wenye anuani (pambio) ya (Salaaman yaa Hussein) yakafuatia maonyesho ya picha za baadhi za harakati za shule, halafu ukafuata ujumbe wa kitengo cha malezi na elimu ya juu ulio wasilishwa na dokta Jaasim Said Ibrahimiy alisema kua: “Hakika kazi ya malezi na kufundisha ni kazi tukufu, ni kazi ya manabii na mitume (a.s), ndio maana Atabatu Abbasiyya tukufu imeanzisha miradi ya malezi na kufundisha, miongoni mwa miradi hiyo ni shule za Abulfadhil Abbasi (a.s) zinazo lenga kupokea wanafunzi wa viwango vyote, kuanzia chekechea hadi chuo, wakitumia vifaa vya kufundishia vya kisasa zaidi vinavyo mjenga mwanafunzi kiakili na kumfanya afaulu zaidi”.

Akaongeza kua: “Leo tunafanya hafla ya kufikisha miaka ya kuwajibikiwa na sheria (kubalekhe) kwa wanafunzi wetu watukufu walio fika umri huo, ili wajiandae na hatua mpya katika maisha wao, pia tunazindua mashindano ya kielimu na maktaba ya shule, vitakavyo changia katika kuwajenga kifikra na kiakili”.

Baada ya hapo wanafunzi walionyesha kazi mbalimbali likiwemo igizo la (Muhammad mkazi) na wakasoma qaswida za kimashairi pamoja na ngonjera ya (Mola amenitukuza kwa kunipa majukumu), kisha wakaswali Magharibi kwa jamaa na wakasoma surat Qiyamah, hafla ikamaliziwa kwa kugawa zawadi kwa wanafunzi walio fika umri wa kuwajibikiwa na sheria (balekhe) na baadhi ya walimu, kisha wahudhuriaji wakaelekea katika uzinduzi wa mashindano ya kielimu yaliyo husisha somo la (Kemia, Fizikia na Sayansi) pamoja na uzinduzi wa maktaba ya shule.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: