Atabatu Abbasiyya yafanya hafla ya Qur’an na kumaliza semina ya imamu Jawaad (a.s) iliyo endeshwa na Maahadi ya Qur’an tukufu..

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa imamu Jawaad (a.s) na ushindi mkubwa walio pata kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, kituo cha kuandaa wasomi na mahafidh wa Qur’an tukufu kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu alasiri ya Juma Pili (11 Rajabu 1438 h) sawa na (9 April 2017 m) wamefanya hafla ya Qur’an tukufu na kuhitimu kwa walimu (40) katika Maahadi ya Qur’an (tawi la India) walio shiriki katika semina ya imamu Jawaad (a.s) iliyo endeshwa na kituo hiki kwa kushirikiana na msomaji wa Qur’an kutoka katika Atabatu Radhawiyya tukufu Shekh Haamid Shaakir Najad, Maahadi ya Qur’an tukufu ilitoa mualiko rasmi kwa wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) kutokana na ushindi wanao pata dhidi ya magaidi ya Daesh.

Hafla ilifanyika katika ukumbi wa haram tukufu ya Abbasi (a.s) na ilihudhuriwa na kiongozi mkuu (mushrifu) wa kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) na kundi kubwa la waumini, ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, kisha akaongea kiongozi mkuu wa kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s), Ustadh Maitham Zaidiy, miongoni mwa aliyo sema ni: “Hakika kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) ni mbegu njema iliyo tokana na fatwa tukufu ya kujilinda, na imetokea katika Ataba hii takatifu, viongozi wengi wa kikosi hicho ni makamanda wa Ataba tukufu na watumishi wake, wamejitolea kila walicho nacho katika uwanja wa vita kwa ajili ya nchi hadi baadi yao wamepata shahada”.

Akaoneza kua: “Ndugu zangu watukufu kwa haraka haraka nakuambieni baadhi ya harakati za kikosi hiki, ambacho kimepata ushindi sehemu nyingi za vita kilizo shiriki, kama vile vita ya mji wa Jurfu Naswir, Aamiriliy, Sayyid Gharib, Dujail, Balad, Samaraa, Tikrit hadi katika ushindi mtukufu ambao tutafanya kumbukumbu yake muda mfupi ujao, ushindi wa mji wa Basheer, mji huo madhulimu watu wake waliomba kuokolewa kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) kikaitikia wito wao”.

Akaendelea kusema kua: “Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kimepata heshima ya kua wawakilishi pekee wa Hashdi Sha’abi katika vita vya kukomboa upande wa kulia wa mji wa Mosul, kinashirikiana na jeshi la Iraq bega kwa bega, kimepata mafanikio makubwa sana, kimekomboa zaidi ya kilometa (300) ndani ya siku (30) na kimeua zaidi ya magaidi (420) sasa hivi tunajiandaa kukamilisha kazi tuliyo anza ya kulinda nchi kwa kushiriki katika vita ya kukomboa mji wote wa Tal-afar”.

Baada ya hapo wahudhuriaji walisikiliza kisomo cha Qur’an tukufu kutoka kwa Falaah Zalif na Haamid Shaakir Najad, hafla ilihitimishwa kwa kugawa zawadi na vyeti kwa washiriki wa semina.

Sayyid Hasanain Halu mkuu wa kituo cha kuandaa wasomi na mahafidh wa Qur’an tukufu aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Leo tumefanya hafla hii kwa mnasaba wa kuzaliwa imamu Jawaad (a.s) na kufatia mafanikio ya kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, vilevile kwa mnasaba wa kuhitimu walimu wa Qur’an tukufu wa tawi la Maahadi ya Qur’an chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kutoka India, hafla imehudhuriwa na wasomi na mahafidh wa Qur’an tukufu akiwemo Shekh Haamid Shaakir Najad kutoka jamuhuri ya kiislamu ya Iran, semina ilikua na mihadhara (20) takriban, katika kila wiki muhadhara mmoja, wamehitimu walimu (40) na zitafuatia semina zingine zitakazo kua na mihadhara tofauti inshallah.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: