Kusimama katika matatizo ya vijana na utatuzi wake: Idara ya masomo na usambazaji ya Atabatu Abbasiyya tukufu imeweka mikononi mwa wasomaji vitabu vinavyo elezea (kujenga shakhsiya yenye mafanikio)..

Maoni katika picha
Kubadilika kifikra, kitamaduni na kimwenendo kwa mwanadamu kunahitaji mambo mengi na muhimu baada ya kuchunguza matatizo na mazingira tofauti, kwa kua Atabatu Abbasiyya ililipa jambo hili umuhimu mkubwa kupitia machapisho na tungo zake zinazo lenga watu wa tabaka zote kuanzia watoto hadi umri wa balekhe, hivyo ilikua hakuna budi ya kutoa vitabu vitakavyo angazia mambo haya, ndio umetolewa mtiririko wa vitabu vya (Kujenga shakhsiya yenye mafanikio) vilivyo tolewa na idara ya masomo na usambazaji chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Ataba tukufu.

Ili kufahamu zaidi, mtandao wa Alkafeel umeongea na muandishi wa vitabu hivyo Ustadh Hassan Ali Jawadiy alikua na haya ya kusema: “Kama mnavyo fahamu mwanadamu ni kiumbe mwenye akili zaidi miongoni mwa viumbe waliopo duniani, hakuna kiumbe anaye starehe na akili kama mwanadamu, hivyo kazi ya kubadilisha kiakili na utamaduni wa mtu inahitaji mambo mengi, kutokana na msingi huo tumeandika vitabu hivi na kuvipa jina la (Kujenga shakhsiya yenye mafanikio) fikra ya kuandika vitabu hivi ilikuja baada ya mawasiliano ya karibu na vijana pamoja na kuishi nao kwa muda fulani na kufahamu matatizo na changamoto wanazo kutana nazo kuanzia siku ya kwanza hadi siku ya mwisho wa ujana wao, ili viweze kukidhi haja kwa kiasi fulani kuhusu kuelezea dunia ya vijana”.

Akaongeza kua: “Hakika lengo la kuandika vitabu hivi ni kuangazia matatizo ya vijana na kuangalia utatuzi wake na kuwajenga kifikra, kitamaduni na kiimani kwa upande mwingine, tumetumia njia ya kutoa fikra na kujadili visababishi, kwa kusajili vitendo na mambo yanayo pewa umuhimu na vijana, tumeandika mambo mengi yanayo pewa umuhimu na vijana wa zama hizi, nimetilia msisitizo katika kuelezea sifa nzuri zinazo jenga shakhsiya njema ya mwanadamu, pia nimeelezea mambo ya kufikirika (kubuni) ambayo hukwamisha maendeleo ya mwanadamu, pia tukalenga kuondoa utata unao weza kukwamisha maendeleo”.

Kuhusu idadi ya vitabu hivyo Ustadh Jawadiy alisema kua: “Hadi sasa mtiririko huu umefika matoleo sita, kila moja limeelezea mada tofauti kuhusu ujengaji wa shakhsiya, kama ifuatavyo:

Toleo la kwanza lilikua mwaka (2014 m) likiwa na anuani isemayo: (Kujenga shakhsiya baina ya uhakika na utata) lilikua na mada nyingi muhimu kwa vijana, lilitumia lugha iliyo karibu na fikra za vijana, toleo hilo lilijikita katika kuelezea zaidi nukta mbili muhimu ambazo ni: Nyenzo za kujengea shakhsiya ya hakika (nzuri) na nyenzo za kujengea shakhsiyya tata (mbaya).

Toleo la pili lilikua na anuani isemayo: (Urafiki katika ulimwengu mpana) lilibeba mada nyingi zilizoelezea urafiki, likajikita zaidi katika kuelezea mafuhumu ya undugu na uhusiano baina ya mtu na mtu, na likabainisha alama za rafiki wa kweli (mwema) anaye kusudiwa na riwaya za Ahlubait (a.s).

Toleo la tatu lilikua mwaka (2015 m) likiwa na anuani isemayo: (Chagua shakhsiya yako) lilibainisha shakhsiya nzuri na mbaya, na kuzielezea kwa kina, lilijikita zaidi katika kuchambua aina za shakhsiya moja moja na mazuri na mabaya yake.

Toleo la nne lilielezea maisha ya vijana na wanadamu kwa ujumla, lilikua na anuani isemayo: (Uzuri katika mtazamo wa kimaada na kimaana) lilielezea mafuhumu ya uzuri wa kweli na aina zake, likibainisha kua watu huangalia uzuri wa mtu kwa kigezo cha sura na mali zake, wakati kuna uzuri wa roho na wakimaana (usio wa vitu vya kuonekana).

Toleo la tano lilikua na anuani isemayo: (Kanuni za kufaulu) lilibeba utatuzi wa changamoto nyingi, lilielezea zaidi namna ya kuishi na watu.

Toleo la sita lilikua na anuani isemayo: (Uelewa na utambuzi katika kuvunja kioo cha utata) toleo hili limejadili mitazamo hasi (mibaya) inayo mtoa mwanadamu katika lengo sahihi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: