Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya mazoezi hai kwa wahitimu wa kozi ya utoaji wa huduma ya kwanza (uokozi)..

Maoni katika picha
Kitengo cha mipango na maendeleo ya mwanadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu jana Juma Tatu (12 Rajabu 1438 h) sawa na (10 April 2017 m) wamefanya mazoezi hai kwa wahitimu wa kozi wa utoaji wa huduma ya kwanza wa awamu ya (nane, tisa na kumi) zilizo endeshwa na idara ya afya kwa wafanyakazi wa Ataba tukufu, ambayo ilijikita katika namna ya kukabiliana na majanga, majeraha na moto, kozi hizi ni kwa ajili ya kuongeza kiwango cha watumishi katika kukabiliana na mazingira hayo ambayo hutokea vitani mara nyingi na hata katika maisha ya kawaida.

Mazoezi hayo yalifanywa takriban na wahitimu (45), yalihudhuriwa na chama cha mwezi mwekundu tawi la Karbala, ujumbe wa kitengo cha mipango na maendeleo ya mwanadamu ambao ndio wasimamizi wa kuu wa kozi hii uliwasilishwa na Shekh Mustafa Idani, ambaye alipongeza kozi hizi na kuelezea umuhimu wake katika kusaidia majeruhi.

Akaongeza kua: “Hakika kazi za Ataba tukufu sio kutoa huduma za afya na malezi peke yake, bali inatilia umuhimu pia maswala ya kusaidia majeruhi na wahanga wa ugaidi kwa kuwafundisha watumishi wake mbinu za uokozi, hii yote inaonyesha juhudi zinazo fanywa na Ataba tukufu katika upande wa ubinadamu”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya huendesha kozi za kutoa huduma ya kwanza kwa watumishi wake kila baada ya muda fulani, kwa ajili ya kuongeza uwezo wao wa kupambana na mazingira hatari kama yakitokea, sawa iwe katika maisha ya kawaida au vitani, kitengo cha mipango na maendeleo ya mwanadamu kimechangia kwa kiasi kikubwa kutoa mafunzo hayo kwa watumishi wa Ataba tukufu, mafunzo ya namna ya kuokoa majeruhi katikati ya milio ya risasi, kutibu majeruhi, pamoja na kuunda kitengo cha uokozi (huduma ya kwanza) na kuwafundisha mbinu za kisasa, juhudi hizi zimepelekea kuhitimu kwa idadi kubwa ya watumishi kutoka katika vitengo mbalimbali vya Ataba tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: